Jumapili 28 Desemba 2025 - 23:00
Mazishi ya Mwanazuoni Sheikh Ridha Mahmoud Mahdi, yafanyika katika mji wa Khartoum nchini Lebanon

Hawza/ Hizbullah na watu wa Muqawama waliuaga mwili wa Mwanazuoni, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Ridha Mahmoud Mahdi.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hizbullah na watu wa Muqawama waliuaga mwili wa Mwanazuoni Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Ridha Mahmoud Mahdi, ambaye hivi karibuni alifariki dunia baada ya maisha marefu aliyoyatumia katika nyanja za elimu na jihadi.

Hafla ya mazishi ya Sheikh Mahdi ilianza katika mji wake alio zaliwa wa Khartoum, na ilifanyika kwa ushiriki wa watu mashuhuri wa kisiasa, kitamaduni, kidini, kiharakati na kielimu, pamoja na wanazuoni wa dini, wanaharakati wa kijamii, na umati mkubwa wa wakazi na wapenzi wa marehemu.

Msafara wa mazishi uliendelea kupitia barabara za miji kuelekea makaburi ya (al-Jabbāna), ambapo mwili wa marehemu uliswaliwa, kisha akazikwa katika ardhi tulivu, kwa kumuaga kwa heshima inayostahili safari yake ndefu ya kujitolea.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha