Jumatatu 29 Desemba 2025 - 00:00
Kunyongwa vijana 3 wa Kishia hivi karibuni huko Qatif ni jinai ya kisiasa na ukiukwaji wa wazi wa haki

Hawza/ Jumuiya ya Amal ya Kiislamu ya Bahrain katika taarifa yake imeainisha kuwa: Kunyongwa kwa Sayyid Hussein Al-Qallaf, Muhammad Ahmad Al-Hamad na Hassan Saleh Al-Salim, waliokuwa wakizuiliwa kutoka Qatif na utawala wa Saudi, katika siku za mwisho za mwaka wa kalenda ya Miladia, ni jinai kamili ya kisiasa.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, katika mwendelezo wa uhalifu unaofanywa na utawala wa Aal-Saud dhidi ya Waislamu wa Kishia wa Saudi Arabia, na katika siku za mwisho za mwaka wa Miladia sambamba na wiki ya kumbukumbu ya shahidi Ayatullah Nimer — aliyefikia daraja ya shahada miaka kumi iliyopita kwa mkono wa utawala wa Aal-Saud — habari za kunyongwa vijana wengine watatu wasio na hatia wa Qatif zilisambaa kwwnye mitandao ya kijamii.

Jumuiya ya Amal ya Kiislamu ya Bahrain, kupitia taarifa yake, huku ikilaani vikali uhalifu huu wa kinyama, imyataka mashirika ya haki za binadamu na mamlaka husika katika ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu kuchukua hatua za kivitendo.

Maandishi ya taarifa ya Jumuiya ya Amal ya Kiislamu ya Bahrain ni kama ifuatavyo:

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيمِ

إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَیْهِ رَاجِعُونَ

وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِینَ قُتِلُوا فِی سَبِیلِ اللَّهِ أَمْوَاتًا بَلْ أَحْیَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ یُرْزَقُونَ
(Wala usiwadhanie wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa wamekufa; bali wao wako hai mbele ya Mola wao wanaruzukiwa)

Jumuiya ya Amal ya Kiislamu ya Bahrain inaeleza kwa masikitiko na huzuni nyingi kabisa, sambamba na kulaani na kukemea kwa nguvu zake zote, mwendelezi wa ukiukwaji wa kimfumo na mzito dhidi ya watu wa Qatif, katika kipindi cha kuelekea kumbukumbu ya miaka kumi ya huzuni ya shahada ya mwanazuoni mujahidi, Ayatullah Sheikh Nimer Baqir Al-Nimer (ra).

Kuuawa kwa shahidi Ayatullah Nimer lilikuwa tukio la kihistoria na la kuamua hatima, lililofichua wazi mkondo wa dhulma, udikteta na jitihada za kuzima sauti huru zinazodai haki na utu.

Kunyongwa kwa Sayyid Hussein Al-Qallaf, Muhammad Ahmad Al-Hamad na Hassan Saleh Al-Salim, waliokuwa wakizuiliwa kutoka Qatif na utawala wa Saudi, siku ya Jumanne tarehe 23 Desemba 2025, ni jinai kamili ya kisiasa.

Kwa mujibu wa taarifa hii, Jumuiya ya Amal ya Kiislamu ya Bahrain imesisitiza kuwa; uwajibikaji kamili wa uhalifu huu unawaangukia viongozi wa sasa wa utawala wa Aal-Saud, na kwamba huu ni ukiukaji wa wazi wa haki na mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu, na tunasisitiza tena kuwa matumizi ya kulipiza kisasi, adhabu ya pamoja na usafishaji wa kisiasa ni mbinu zinazotumiwa kudhibiti migogoro ya ndani.

Jumuiya ya Amal ya Kiislamu ya Bahrain inaamini kuwa, mbinu hizi haziwezi kutenganishwa na muktadha mpana wa sera za ubaguzi, kutengwa na kuwekewa mipaka uhuru ya kidini na kisiasa; sera ambazo hulenga kundi maalumu kwa misingi ya madhehebu na misimamo ua kisiasa, na ambazo ni ukiukwaji wa wazi wa misingi ya usawa ua uraia na viwango vya msingi kabisa vya dola yenye haki.

Jumuiya ya Amal ya Kiislamu ya Bahrain, huku ikisisitiza tena msimamo wake usiotetereka wa kuunga mkono malengo ya watu waliodhulumiwa wa eneo hili, inaiona mataifa kunyamaza mbele ya uhalifu huu kuwa ni ushirika wa moja kwa moja katika kuendelezwa kwake, na inaiwajibisha jumuiya ya kimataifa — hususan madola makubwa, wanachama wa Baraza la Usalama, mashirika ya haki za binadamu pamoja na Umoja wa Mataifa — kwa kushindwa kuchukua hatua madhubuti za kukomesha ukiukaji huu na kuwawajibisha wahusika wake.

Jumuiya hii pia inaziomba nguvu za kisiasa na kidini pamoja na mashirika ya haki za binadamu duniani kote, hasa katika ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu, kuchukua misimamo iliyo wazi na yenye kuwajibika, ili kusaidia kulinda haki halali za watu, kuimarisha misingi ya haki, uhuru na utu wa kibinadamu, na kukomesha mauaji ya kimfumo yanayotekelezwa na utawala wa Aal-Saud.

Jumuiya hii inatoa rambirambi zake za dhati kabisa na mshikamano wa kweli katika janga hili kubwa kwa familia za mashahidi wema, jamaa na wapendwa wao, kwa watu wenye heshima wa Qatif na kwa watu wote huru, na inamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awajalie mashahidi rehema Zake pana, aifanye damu yao kuwa nuru ya njia ya haki na daraja la kufikia matakwa ya haki, na awape familia na wapendwa wao subira, utulivu na uimara.

Amani iwe juu ya mashahidi; siku walipozaliwa, siku walipouawa kishahidi, na siku watakapofufuliwa wakiwa hai.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha