Jumapili 28 Desemba 2025 - 23:30
Muqawama unaendelea kwa nguvu hadi itakapotimia ahadi ya Mwenyezi Mungu / Maktaba ya Shahidi Suleimani ni nguzo ya kifikra kwa Muqawama wa Kiislamu

Hawza/ Hujjatul-Islam Sheikh al-Baghdadi alisisitiza kuwa: Muqawama unaendelea kwa nguvu na kwa kushikamana na maktaba ya mashahidi na uongozi, katika njia ya kusimama imara na kupambana na adui hadi kutimia kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Mashhad Iran, Hujjatul-Islam Sheikh Hassan al-Baghdadi, mjumbe wa Baraza Kuu la Hizbullah Lebanon, jioni ya Jumamosi tarehe 27 December , katika Kongamano la Pili la Kimataifa la al-Ghalibun lenye kichwa cha habari kisemacho “Maktaba ya Shahidi Suleimani; Njia Iliyowazi ya Muqawama”, lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli Aftab-e-Welayat, alifafanua misingi ya kifikra na kimkakati ya Muqawama, na akasisitiza juu ya kuendelezwa kwa njia ya mashahidi hadi kutimia kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu.

Akiwashukuru waandaaji wa kongamano hili la kimataifa kwa kuhuisha kumbukumbu ya hadhi tukufu ya Shahidi Hajj Qassem Suleimani, alitoa pongezi kwa juhudi zilizofanyika katika kuandaa tukio hili la kielimu na kitamaduni, na akawasilisha salamu za Katibu Mkuu wa Hizbullah Lebanon, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Naim Qassem, pamoja na wapiganaji wa Muqawama, kwa wanazuoni, wasomi na wahudhuriaji.

Shahidi Suleimani, alama ya uaminifu kwa maktaba ya Imamu na uongozi

Mjumbe wa Baraza Kuu la Hizbullah Lebanon, akirejea haiba ya kipekee ya Shahidi Hajj Qassem Suleimani, alisema: Shahidi Suleimani alikuwa mfano halisi wa kushikamana na maktaba ya Imamu Khomeini (rehma ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake) na utiifu wa vitendo kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu; na njia ya Muqawama wa Kiislamu, chini ya uongozi wa maktaba hii yenye nuru, inaendelea kwa nguvu zaidi.

Akirejea nafasi ya msingi ya Hizbullah katika kukabiliana na mipango ya kiutawala ya Magharibi, alisisitiza: tumesimama mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni na mradi wa “Mashariki ya Kati Mpya”; mradi ambao lengo lake lilikuwa ni kupora rasilimali za mataifa, kuvunja utambulisho wa Kiislamu na kuimarisha utawala wa Marekani na utawala wa Kizayuni katika eneo hili, lakini kwa msimamo wa Muqawama, mradi huo ulishindwa.

Hujjatul-Islam Sheikh al-Baghdadi, akirejea mapambano yasiyo na uwiano kati ya Muqawama na utawala wa Kizayuni, alisema: katika vita ambavyo adui aliingia uwanjani kwa kuhamasisha zaidi ya wanajeshi elfu 75 pamoja na uwezo wake wote wa kijasusi na kijeshi, wapiganaji wa Muqawama hawakurudi nyuma hata kwa muda mfupi, bali kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu, walimlazimisha adui kurudi nyuma na kukubali kushindwa.

Aliongeza kuwa: baada ya wiki kadhaa za mapambano makali, utawala wa Kizayuni ulilazimika kusalimu amri mbele ya makubaliano na mifumo iliyopendekezwa na Muqawama katika uwanja wa kimataifa, na huu ni ushahidi wa wazi wa irada ya Muqawama.

Adui ashindwa kuudhoofisha Muqawama baada ya kuuawa kishahidi makamanda

Mjumbe wa Baraza Kuu la Hizbullah Lebanon, akirejea kuuawa kishahidi kwa makamanda mashuhuri wa Muqawama, alisema: adui alidhani kwamba kwa kuuawa kishahidi viongozi na makamanda wa Muqawama, harakati hii ingedhoofika, lakini damu ya mashahidi ilileta mshikamano, nguvu na uhai zaidi kwa Muqawama, na ikavuruga kabisa hesabu zote za adui.

Subira, imani na kutimia kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu

Akinukuu Aya Tukufu «وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ», alisisitiza kuwa: Mataifa na wapiganaji wa Muqawama walisimama imara mbele ya misukosuko mikubwa zaidi, na kwa imani ya «إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ», walizitoa roho, mali na heshima zao, na wakaonesha kutimia kwa ahadi ya nusra ya Mwenyezi Mungu katika uwanja wa vitendo.

Ushindi au shahada; mantiki isiyobadilika kwa Muqawama 

Hujjatul-Islam Sheikh al-Baghdadi alisema: Kwa wapiganaji wa njia ya Mwenyezi Mungu, daima kuna hatima moja kati ya mbili; ima shahada, ambayo ni kilele cha heshima, au ushindi katika uwanja wa mapambano, na katika hali zote mbili, Muqawama huwa mshindi na wenye heshima.

Akirejea vita vya hivi karibuni, alisema: lau utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake wangekuwa washindi, bila shaka wangetoa ripoti rasmi na zenye vielelezo kuhusu ushindi wao; lakini ukimya wa vyombo vya habari na kuficha ukweli kwao, ni dalili ya wazi ya kushindwa kwao na hasara kubwa walizopata.

Onyo la wazi kwa Marekani na utawala wa Kizayuni

Mjumbe wa Baraza Kuu la Hizbullah Lebanon alisema: Iwapo Marekani na utawala wa Kizayuni wanakusudia kurudia vita, basi na wajiribu, ili waone tena jinsi Muqawama unavyoitetea ardhi, heshima na uwepo wake, na jinsi unavyomwangusha adui katika uwanja wa mapambano.

Akirejea hali ya sasa ya ulimwengu wa Kiislamu, aliongeza: leo pia, kama ilivyokuwa katika vita vya Ahzab, maadui wote wa Uislamu wameungana kwa lengo la kuuangamiza, lakini kama ilivyotokea katika historia ya Uislamu ambapo nguvu ya maadui ilivunjwa, safari hii pia, kwa mkono wa kiongozi mwenye hekima na kamanda shujaa wa Umma wa Kiislamu, kushindwa kwao kwa mwisho kutalazimishwa.

Kuendelezwa kwa njia ya Muqawama hadi kutimia kwa ahadi ya mwisho

Hujjatul-Islam Sheikh al-Baghdadi alisisitiza: sisi ni warithi wa kweli wa maktaba ya Amirul-Mu’minin Ali (amani iwe juu yake), na tutaendelea na njia hii kwa imani, basira na subira hadi kutimia kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu na kuandaa mazingira ya kudhihiri Imam wa Zama, Hujjat bin al-Hasan (a.f.), kwa nguvu na uthabiti.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha