Jumamosi 27 Desemba 2025 - 11:49
Shahidi Ayatullah Hakim alikuwa na mchango mkubwa katika kuasisiwa demokrasia ya Iraq

Hawza/ Karam al-Khaz‘ali, mjembe wa Harakati ya Hikmat ya Kitaifa ya Iraq, alisisitiza kuwa; Shahidi wa Mihrabu, Ayatullah Sayyid Muhammad Baqir al-Hakim, alitoa mchango mkubwa na wa kipekee katika kuasisiwa demokrasia ya Iraq mpya.

Kwa mujibu wa ripoti ya idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Karam al-Khaz‘ali, mjumbe wa Harakati ya Hikmat ya Kitaifa ya Iraq, alisisitiza kuwa Shahidi wa Mihrabu, Ayatullah Sayyid Muhammad Baqir al-Hakim, alicheza jukumu muhimu na la kipekee katika kuasisiwa kwa demokrasia ya Iraq mpya.

Al-Khaz‘ali alisema: Shahidi wa Mihrabu aliacha urithi wa kudumu katika jihadi na muqawama dhidi ya udikteta. Alianza maisha yake katika mji mtukufu wa Najaf kwa kutafuta elimu, kisha akageuka kuwa msomi, mujtahidi, mpambanaji na hatimaye shahidi.

Aliongeza kusema: Shahidi wa Mihrabu, kama babu yake Imam Hussein (amani iwe juu yake), alisimama imara dhidi ya dhulma na madhalimu, akaikataa batili, na akaingia katika mapambano dhidi ya udhalimu na udikteta.

Al-Khaz‘ali alibainisha kuwa ujasiri aliokuwa nao shahidi wetu wa milele umeendelea kubaki hadi leo ndani ya Iraq mpya kama alama na ishara, na kwamba maneno yake yote daima yalikuwa yakihimiza umoja na uzalendo; na kwamba kukosekana kwake ni pigo kubwa sana kwetu.

Mwisho alisema: Shahidi Ayatullah al-Hakim alikuwa na mchango mkubwa zaidi katika kuasisiwa demokrasia katika Iraq mpya na katika mchakato wa kisiasa, na daima alikuwa akituhusia kwenda sambamba na ustaarabu huku tukibakie waaminifu kwenye mafundisho na kufanya ibada, hii ilimfanya awe kiongozi wa mfano na shahidi kwa wakati mmoja.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha