Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, awamu ya pili ya kongamano la kimataifa la kuadhimisha miaka mia moja ya kuanzishwa upya kwa Hawza ya Qom limefanyika alasiri ya leo katika ukumbi wa mikutano wa Madrasa ya Imamu Kādhim (a.s.).
Katika kongamano hili tulishuhudia kutolewa kwa ujumbe wa Ayatollah Nūrī Hamedānī, ambao matini yake ni kama ifuatavyo:
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمنِ الرَّحِيمِ
الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِینَ وَ الصَّلَاةُ وَ السَّلَامُ عَلَی سَیِّدِنا وَ نَبِیِّنَا أَبِی الْقَاسِمِ المصطفی مُحَمَّد وَ عَلَی أهلِ بَیتِهِ الطَّیِّبِینَ الطَّاهِرِینَ سیَّما بَقیَّهَ اللهِ فِی الأرَضینَ.
«وَمَا کَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِیَنفِرُوا کَافَّةً فَلَوْلَا نَفَرَ مِنْ کُلِّ فِرْقَةٍ مِنْهُمْ طَائِفَةٌ لِیَتَفَقَّهُوا فِی الدِّینِ وَلِیُنذِرُوا قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُوا إِلَیْهِمْ لَعَلَّهُمْ یَحْذَرُونَ.»
Na si kwamba Waumini wote wanapaswa kutoka (kwenda vitani); basi kwa nini lisitoke kundi katika kila jama‘a miongoni mwao ili wapate uelewa mzuri katika dini, na wawaonye watu wao wanaporudi kwao huenda wakajihadhari. (At-Tawba: 122)
Kwa salamu na heshima, mkutano huo tukufu unaoendelea kwa kuhudhuriwa na maulamaa, wanavyuoni na shakhsia mashuhuri zenye athari.
Mwanzilishi wa Hawza ni Mola Mlezi ambaye kwa mara ya kwanza alitoa amri ya kusafiri kwa kikundi cha Waislamu kutoka miji mbalimbali kuelekea kwenye kituo cha elimu, na akaweka utaratibu kwamba baada ya kupata elimu katika kituo hicho cha fadhila, warudi kwao na kuwaonya kaumu yao.
Mtume mtukufu wa Mwenyezi Mungu (saw) anapaswa kuchukuliwa kuwa ndiye muanzilishi wa kwanza wa hawza, ambaye aliifanya mji wa Madina kuwa kituo cha elimu na fadhila, ili watafutaji wa maarifa kutoka miji mbalimbali waelekee katika ardhi hiyo ya nuru, na baada ya kupata elimu na kujisafisha, warudi kuwaongoza kaumu zao.
Maimamu wa Kishia ambao baada ya hapo waliibadilisha miji kama Kufa, Madina, na Baghdad kuwa vituo vya elimu na malezi ya wanazuoni wacha Mungu, wao pia ni miongoni mwa waanzilishi wa Hawza. Huenda ni kwa sababu hii ndipo ambapo katika zama za ghaiba, Hawza za Kishia za Imamiyya katika miji kama Najaf, Samarra, Mashhad na Qom ziliota mizizi, zikakua na kutoa matunda kwa kuzunguka makaburi yenye nuru ya kizazi hiki kitukufu.
Moja kati ya Hawza hizi ni Hawza ya Qom, ambayo miaka mia moja iliyopita, katika moja ya nyakati ngumu zaidi katika historia ya Iran, ilianzishwa kwa busara na hekima ya Ayatollah al-‘Udhma Shaykh ‘Abdulkarīm Ḥā’irī Yazdī (ra), kwa mtazamo wa kina lakini wa utulivu na tahadhari dhidi ya siasa zenye kupinga dini zilizokuwepo wakati huo.
Mtazamo huo wa kisiasa uliokuwa umepuuzwa ndani kwa ndani katika nafsi ya Sheikh Muasisi (ra), ulikuwa umefungamana na hatima ya kisiasa ya Uislamu na Ushia na nafasi yake katika ulimwengu wa kisasa, na kwa hatua kwa hatua, kupitia juhudi za kielimu na kivitendo za wanazuoni wakubwa kama Ayatollah al-‘Uzma Burūjerdī na wanafunzi wake wapiganiaji, ukabadilika na kuwa "mti mzuri" ambao:
تُؤْتِي أُكُلَهَا كُلَّ حِينٍ بِإِذْنِ رَبِّهَا
"Hutoa matunda yake kila mara kwa idhini ya Mola wake." (Ibrāhīm: 25)
Hujjatul-Islam Sheikh (ra), kwa mtazamo wake wa mbali, aliliasisi chuo hiki kitukufu kwa namna ambayo kisihitimishe utekelezaji wa fadhila za kielimu tu ndani ya jihadi kubwa (الجهاد الأكبر), bali kiingie kwa wakati unaofaa katika uwanja wa jihadi ndogo (الجهاد الأصغر), na kwa kuvumilia mashaka yasiyo na idadi na kumwaga damu safi, kitoe maana kwenye harakati za wananchi wa Iran waliokuwa wakidai haki na uadilifu. Na kikaendeleza mapambano hayo hadi ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuasisiwa kwa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Katika mchakato huu, nafasi ya Imam Khomeini (ra) ilikuwa ya kipekee na isiyosahaulika.
Leo hii, ambapo mti huu mtukufu wa heri (الشجرة الطيبة) umepita njia yenye mikunjo mingi na mwinuko na hatimaye kufikia miaka mia moja ya uhai wake, ni wajibu kwa maulamaa wakubwa kuishika mikono ya vijana wa chuo hiki, wasimame pamoja juu ya kilele cha mafanikio haya ya karne moja, waelekeze macho yao kwa pamoja katika upeo wa mbele, na waweke mambo kadhaa mbele ya macho yao:
Kwanza, wautambue upya urithi wa asili, thabiti na usiobadilika wa chuo, na waweke tofauti na mila na ada zinazobadilika kwa mujibu wa hali na wakati. Hii ni kwa namna ambayo hakuna uzembe katika kulinda misingi hiyo thabiti ya kielimu, wala kusikitikia kuachana na desturi zinazopaswa kubadilika kwa mujibu wa muktadha wa wakati.
Kisha, kwa kushikamana na misingi hiyo ya asili ya chuo, waangalie pia hali halisi ya kisasa na wafahamu kwa undani mahitaji ya ulimwengu wa leo bila ya kuangalia mambo juu juu, ili chuo hiki kisije kikajikuta, bila kukusudia, kikielekea kwenye kujitenga na kujitenga huko hakutakuwa na mwisho isipokuwa kuyeyuka taratibu.
Na jambo jingine muhimu ni kwamba elimu na maarifa ya thamani ya chuo hiki – ambayo ni hazina ya maswali na juhudi za zaidi ya miaka elfu moja na mia nne ya ustaarabu wa Kiislamu na Kishia – yasitolewe kwa thamani yoyote ile, lakini wakati huo huo yawe na uangalizi wa kila siku juu ya mahitaji ya ulimwengu, mahitaji ya Waislamu na Mashia duniani, na mahitaji ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu. Maarifa haya yafafanuliwe upya na yazalishwe kwa namna ambayo yaweze kujibu mahitaji ya sasa.
Na jambo la msingi zaidi ni kwamba mhimili mkuu wa maarifa ya kielimu ya chuo hiki ni Qur'an Tukufu na Sunna ya Mtume na Ahlul Bayt watakatifu – amani iwe juu yao wote – lakini ili maarifa haya yasipotoshwe kwa kupindukia au kwa kupunguzwa, haipaswi kusahaulika nafasi ya ‘akili’ kama hoja ya kimungu pamoja na vyanzo hivyo viwili vya nuru.
Bila shaka, mazingira bora ambayo juhudi hizi zitachipuka humo – na kama mazingira hayo yakipuuzwa basi juhudi hizo hazitazaa matunda – ni maadili, ikhlasi, na kuhisi daima uwepo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Walii Wake Mkuu, Bwana wa Enzi za Nyakati, Imam Mahdi (a.f). Ninatarajia kwamba kipengele hiki cha thamani kitapata nguvu zaidi na kuwa na athari zaidi kadri tunavyosonga mbele kuelekea upeo wa mbele.
Kwa kuhitimisha ni kwamba: Leo hii, Hawza ya Qom, yenye historia ya karne kadhaa, na iliyoanzishwa upya miaka mia moja iliyopita na fakihi mkubwa, Ayatullahil-Udhma Sheikh Abdulkarim Ha’iri Yazdi (rahimahu Allah), inapaswa kufanya shughuli zake kwa namna ambayo vizazi vijavyo vitatambua kuwa uongozi wa kidini wa kweli daima umekuwa pamoja na wananchi, umehisi maumivu yao na umejitahidi kuyapunguza. Mfano wa huduma hizi kwa jamii unaonekana waziwazi, zikiwa ni huduma za manufaa ya umma. Huduma hizo zilitolewa hata katika mazingira magumu ya wakati wa Sheikh Ha’iri mwenyewe, na zimeendelea hadi leo kupitia juhudi za wanachuoni na chuo hiki.
Chuo hiki kimezaa wanafunzi wakubwa, na moja ya matunda yake yalikuwa ni hekima, siasa, busara, na subira ya kiongozi wake mwanzilishi – Sheikh mwanzilishi – ambavyo vilizaa Mapinduzi makubwa ya Kiislamu yaliyofanywa na mmoja wa wanafunzi wake. Mapinduzi hayo yaliufuta kabisa mfumo wa kifalme wa miaka 2500 na kuutupa katika jalala la historia, yakaleta heshima, uhuru na kujitegemea kwa taifa la Iran, na yakaathiri uwanja wa kimataifa kwa namna kubwa. Athari yake ya wazi zaidi ilikuwa ni kutekeleza kivitendo aya za Qur’an Tukufu na hadithi za Ma’asumina, hasa za Amirul-Mu’minin ‘Alayhis Salaam, kuhusu kupambana na dhalimu na kuwatetea wanyonge bila kujali mipaka ya kijiografia. Mapinduzi hayo yameifanya Palestina kuwa suala la kwanza la Uislamu duniani, na kupitia uelimishaji, uhusiano na vyuo vikuu, pamoja na kuwapa vijana nafasi, yamekuwa na athari kubwa – na katika haya yote, chuo cha Qom kimekuwa mstari wa mbele.
Kwa msingi huu, jukumu la kulinda tunda hili kuu, na kulitambulisha pamoja na athari, baraka na mafanikio yake, na vilevile kulifanyia uchambuzi wa madhara, ni juu ya hujra huu tukufu. Kwa kuzingatia waraka wa mwanazuoni uliotumwa leo na Kiongozi mwenye hekima wa Mapinduzi, kwa ajili ya kongamano hili tukufu ambalo linakumbusha Waraka wa kihawza wa Imam Muasisi (ra), waraka huu unaweza kuwa ramani ya njia kwa Hawza, wanafunzi wa elimu ya dini, walimu na wanavyuo mashuhuri. Ninauchukulia mkutano huu adhimu kuwa ni fursa ya thamani, na nawapa heshima na taadhima maulamaa wakubwa waliojitokeza katika kueneza utamaduni wa Qur’an na Ahlul-Bayt waliotakasika na kusafika (as), hasa shakhsia kubwa kwenye zama zetu kama Ayatullah Al-Udhma Hairi, Burujerdi, na Imam Muasisi (ra).
Na mwisho kabisa, nawashukuru na kuwapongeza waandaaji wote wa mkutano huu wa haiba kwa ajili ya mnasaba wa maadhimisho ya miaka mia moja tangu kuanzishwa upya kwa Hawza ya elimu ya dini, ambao kwa muda mrefu walijitahidi kukusanya kazi zenye thamani za marehemu Haj Shaykh, ambapo juzuu 20 tayari zimechapishwa, pamoja na maandiko yanayohusiana na mada hii ikiwa ni pamoja na juzuu 30 za makala zilizokusanywa kwa juhudi kubwa. Ninatoa shukrani maalum kwa usimamizi bora na mwanazuoni mwenye maarifa wa Hawza ya Qom.
Na ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awape wote mafanikio.
Na mwisho wa maombi yetu ni: Alhamdulillahi Rabbil-‘Aalamin.
13 Ordibehesht 1404 (sawa na 3 Mei 2025)
Hussein Nouri Hamedani
Maoni yako