Jumanne 21 Oktoba 2025 - 09:58
Kongamano la Kimataifa linalohusisha Dini Mbali mbali lafanyika katika Mji Mkuu wa Kongo – Kinshasa

Hawza/ Kutokana na juhudi na ufuatiliaji endelevu wa Jumuiya ya Waislamu wa Kishia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – Kinshasa, mkutano mkubwa wa kimataifa kati ya dini mbalimbali uliohusishwa na umoja pamoja na kuishi kwa amani baina ya dini tofauti umefanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, kutokana na jitihada za Baraza Kuu la Waislamu wa Kishia nchini Kongo – Kinshasa, mkutano wa kwanza wa kila mwaka wa mazungumzo baina ya dini tofauti umefanyika katika Msikiti wa Ar-Rasul (s.a.w.w) katika mji mkuu, ukihusisha idadi kubwa ya wanazuoni wa Kiislamu, viongozi wa dini, mapadre, na wawakilishi wa makundi madogo ya kidini. Hafla hiyo ilipata mapokezi makubwa kweye vyombo vya habari vya ndani na vya kikanda.

Aidha, katika hafla hiyo walihudhuria mabalozi wa nchi za Kiislamu kama vile Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Pakistan, Sudan, na Misri, pamoja na baadhi ya wabunge wa Bunge la Taifa na wajumbe wa baraza la mawaziri nchini humo.

Katika sehemu ya hotuba yake, Sheikh Abu Ja‘far ‘Isā Mbākī, Rais wa Baraza Kuu la Waislamu wa Kishia nchini Kongo, aliwakaribisha wageni na washiriki, kisha akatoa taarifa fupi kuhusiana na shughuli pamoja na mafanikio ya baraza hilo katika kipindi cha miaka kumi tangia kuanzishwa kwake, akibainisha kuwa:


“Uislamu ni dini ya huruma na msamaha, na matokeo ya kuukubali Uislamu huu mtukufu ni maisha ya amani yanayoambatana na tamaduni mbalimbali pamoja na kuishi kwa upendo na dini na madhehebu mengine.”

Ni vyema kusemwa kuwa; Baraza Kuu la Waislamu wa Kishia nchini Kongo – Kinshasa, lenye wanachama ishirini wa kudumu, lilianzishwa rasmi mwezi Februari mwaka 2015, na tangia wakati huo limekuwa likiendesha shughuli zake za kidini rasmi. Hivi sasa, baraza hilo linamiliki msikiti na vituo kadhaa vya kiutamaduni katika mji mkuu wa nchi hii, Kinshasa, ambapo zaidi ya waumini 800 wa Kishia wanasimamiwa moja kwa moja, na zaidi ya wengine 3,000 wananufaika kwa njia isiyo ya moja kwa moja kupitia shughuli zinazo endeshwa na jumuiya hiyo ya Kishia mjini Kinshasa.

Kongamano la Kimataifa linalohusisha Dini Mbali mbali lafanyika katika Mji Mkuu wa Kongo – Kinshasa

Kongamano la Kimataifa linalohusisha Dini Mbali mbali lafanyika katika Mji Mkuu wa Kongo – Kinshasa

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha