Jumatano 3 Desemba 2025 - 11:12
Ujumbe Maalumu wa Sheikh Ibrahim Zakzaky kwa Watoto wa Mashahidi Nchini Nigeria

Hawza/ Sheikh Ibrahim Zakzaky katika hotuba yake aliwahimiza watoto wa mashahidi kusimama imara katika njia ya Mwenyezi Mungu, kushikamana na misingi ya jihadi, na kuendeleza mwenendo wa baba zao waliopata shahada. Alisisitiza kuwa damu ya mashahidi ndiyo nguzo ya uamsho, heshima na ushindi wa Umma wa Kiislamu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ibrahim Zakzaky, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria barani Afrika, katika hafla ya kufunga mkutano wa familia za mashahidi uliofanyika Abuja, alizihutubia familia tukufu za mashahidi akiwahimiza kusimama imara katika njia ya haki na kuendeleza njia yenye nuru ya mashahidi. Alisisitiza kuwa njia waliyopita mashahidi ni njia ya imani, ujasiri na ukweli kwa Mwenyezi Mungu, na kwamba warithi wa mashahidi wanapaswa kuendeleza njia hiyo kwa azma thabiti.

Sheikh Zakzaky katika sehemu ya kwanza ya hotuba yake, akirejea mashinikizo na dhulma za maadui, alisema: Maadui wa dini daima hujaribu kwa vitisho na mauaji kuwazuia Waumini wapiganaji wasidumu katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Akikumbushia Siku ya mashahidi”, alisema: Risasi na bunduki hizi zinazolengwa kwetu zinalenga kuwatisha wengine ili wasijiunge nasi. Lakini yeyote anayeogopa mauti, hafai kujiunga na safu zetu; njia hii ni ya wale waliojitolea uhai wao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Waliopo miongoni mwetu lakini wanaogopa kuuawa, wajitenge; kwani uwanja huu si mahali pa hofu wala shaka.

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu aliendelea kwa kusisitiza msimamo imara katika medani ya mapambano kati ya haki na batili, akisema: Sisi si miongoni mwa wale wanaosema ‘njooni mtuue’. Bali sisi tumesimama imara katika njia ya Mwenyezi Mungu, hata kama mwisho wake ni shahada. Anayeogopa, hana nafasi hapa.

Sheikh Zakzaky, akirejea uzoefu wa miaka iliyopita, aliongeza: Ikiwa mtu anataka kututisha, atatumia kitu gani? Kwa risasi? Basi apige! Tayari walishajaribu, na sisi bado tumesimama. Leo hofu imekwisha kabisa; nasi pia tuna shauku ya kufika kule walikofika ndugu zetu mashahidi.

Akiwahutubia madhalimu, alisema: Mmefikia kikomo cha vitisho vyenu kwa kupiga risasi. Sasa mmesalia na nini cha kututisha nacho? Uso wenu wa kweli tayari umefunuliwa.

Alisisitiza kwa kusrma: Familia za mashahidi ambazo mmewanyang’anya wapendwa wao kwa mikono yenu, kamwe hazitawaogopa. Ikiwa kuna wa kuogopa, si wao.

Sheikh Zakzaky katika sehemu nyingine ya hotuba yake alifafanua maana ya “ushindi” na kusema:
Ushindi wa kweli ni mtu kudumu katika njia ya haki hadi afikie mojawapo ya hatima mbili: kufa katika njia ya Mwenyezi Mungu au kupata shahada. Katika hali zote mbili, nusra ya Mwenyezi Mungu hupatikana, na madhalimu kamwe hawatatutawala.

Aliendelea kusema: Ikiwa mtu atakufa katika msimamo, amehitimisha maisha yake katika njia ya haki. Na ikiwa atapata shahada, basi amefikia daraja la juu kabisa katika safari ya kuelekea kwa Mwenyezi Mungu. Hili ndilo “ihda-l-husnayayni” — yaani moja ya mambo mawili mema: ama ushindi au shahada.

Katika sehemu ya mwisho ya hotuba yake, Sheikh Zakzaky kwa kusoma Aya ya 13 ya Suratul-Swaf, alisisitiza juu ya ahadi ya hakika ya nusra ya Mwenyezi Mungu:

“Na jingine mnalolipenda: ni nusra itokayo kwa Mwenyezi Mungu na ushindi ulio karibu; na wabashirie Waumini.”

Akifafanua Aya hii alisema: Nusra hii ni utangulizi wa nusra ya milele; ile “nusra kutoka kwa Mwenyezi Mungu na ushindi wa karibu”, na baada yake, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, huja ahadi ya Pepo zilizo na mito inayopita chini yake. Basi Muumini anawezaje kupuuza mustakabali wa aina hii?

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu akiwahutubia watoto wa mashahidi, alisisitiza kwamba wao wanapaswa kuwa alama ya uthabiti na kutokuwa na hofu: Watoto wa mashahidi wanapaswa kuonesha kuwa damu za baba zao hazikumwagika bure, na kwamba wao bado wamesimama katika ile ile njia. Kusimama imara hadi mwisho wa maisha au kufikia shahada — hatima zote mbili ni kheri na mafanikio.

Aliendelea kwa kukumbusha umuhimu wa matendo mema katika da‘wa ya dini, akisema: Endelezeni ulinganiaji wa dini kwa tabia njema: kwa swala, ibada, adhkari zilizoelekezwa, usafi wa maadili, utiifu kwa Mwenyezi Mungu, na tabia njema. Haiba ya kidini inapaswa ijengwe ndani yenu, kiasi kwamba kila anayewaona, auone Uislamu ndani ya tabia na maneno yenu. Da‘wa ya kweli huathiri pale ambapo maadili na mwenendo wa mtu vinapokuwa kielelezo cha imani na maarifa yake.

Mwisho wa hotuba yake, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu alihitimisha kwa kusema: Jitahidini katika kila jambo kuwa alama na bendera ya dini; kwa hakika roho hii na mwenendo huu ndivyo vitakavyotufikisha kwenye ushindi duniani na Akhera.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha