Jumatano 10 Desemba 2025 - 17:00
Kukosa Usalama na Kutoridhika Ndani ya Mwaka Mmoja wa Utawala wa Jolani Sirya

Hawza/ Katika maadhimisho ya mwaka mmoja tangia kuanguka kwa Bashar al-Assad, iwapo Jolani na timu yake hawataweza kutatua matatizo mengi ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ya Syria na kutoa mtazamo ulio wazi wa kuboresha hali, kuongezeka kwa migogoro ya ndani na kwa upande mwingine kuimarika kwa ubeberu wa Wazayuni, kunaonekana kuwa jambo linalowezekana kabisa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Mohammad Al-Jolani, rais wa kujitangaza wa Syria, hivi karibuni katika mahojiano kwa kisingizio cha kumbukumbu ya kuanguka kwa utawala wa Bashar al-Assad, amesema: “Mwaka uliopita, tulipopata udhibiti wa viunga vya magharibi vya Aleppo, Warusi walituma ujumbe wakisema: simameni hapa tu, shikeni kile mlichokichukua na msiendelee kusonga mbele; la sivyo hali itazidi kuwa mbaya. Nilielewa kuwa utawala ulikuwa umeanguka, kwa hiyo sikujibu chochote na tukaendelea na operesheni, na alhamdulillahi ulikuwa uamuzi mzuri.”

Mwaka mmoja baada ya kuanguka kwa Bashar al-Assad, swali kuu ni hili: kwa hakika Syria inaelekea upande gani, na hatima ya watu wa nchi hii itakuwa ipi!?

Kile ambacho kwa muhtasari kinaweza kusemwa ni kwamba matunda ya utawala wa kiongozi wa magaidi wa jana na kijana mwenye tai wa leo, kinyume na matakwa ya msingi ya watu wa Syria, hayajakuwa yale yanayozunguka maslahi ya taifa la Wasyria; bali kinyume chake, hadi kufikia hapa, mtindo wa siasa wa Jolani umeelekezwa zaidi katika kuhakikisha maslahi ya Marekani, Wazayuni, pamoja na Uturuki.

Hali mbaya zaidi kuliko mwaka mmoja uliopita

Kwa vyovyote vile, kwa mujibu wa wataalamu na wachambuzi wa masuala ya kimataifa, kipindi cha mwaka mmoja ni muda unaofaa kutathmini zama za baada ya Assad; zama ambazo zilipaswa kuwa msimu wa kustawi kwa Syria, lakini inaonekana kuliko wakati mwingine wowote, nchi hii imezama katika migawanyiko na mapigano ya kikabila pamoja na mashindano ya nguvu za kikanda na za nje ya kanda, kiasi kwamba hata usalama wa raia wa kawaida umekuwa mgumu zaidi kwa kiwango kikubwa kuliko kipindi cha utawala wa Assad.

Si ajabu kwamba katika vyombo vya habari daima inasisitizwa hoja kwamba katika hali ya sasa, usalama bado ni kiungo kilichopotea kwa watu wa Syria; mahali ambapo juu angani ndege za kivita za Israel huruka juu ya vichwa vyao, na huku chini ardhini wanakuwa shabaha ya utekwaji nyara na visasi vya kijumuiya na vya umwagaji damu vinavyofanywa na vikosi vinavyohusishwa na Jolani.

Hadithi iliyoanza lakini …

Mwaka uliopita wakati kama huu, waasi na magaidi wa Hay’at Tahrir al-Sham (HTS), mbele ya macho yaliyojaa mshangao ya watu wa dunia na miongoni mwao nchi za eneo la Asia Magharibi, bila upinzani wowote wa maana kutoka kwa jeshi la Syria, ndani ya siku 11 walifika Damascus, na kwa njia hii utawala wa familia ya Assad baada ya nusu karne ukaifikia mwisho.

Bila shaka, tukitazama kwa jicho la haraka mchakato wa mageuzi ya Syria tangu mwaka 2011 hadi sasa, tumeona upangaji mkubwa wa mfumo wa ubeberu na baadhi ya nchi za kanda kwa ajili ya kuidhoofisha na kuigawa Syria kama mojawapo ya nchi muhimu za mhimili wa upinzani; na mwelekeo wa migogoro na fitna katika nchi hii kwa miaka mingi umekuwa kwa namna ambayo misingi ya nchi imeendelea kudhoofishwa na kuchakaa kiasi kwamba mwaka uliopita wakati kama huu, Jolani na wenzake, kwa msaada wa moja kwa moja wa baadhi ya wachezaji wa kikanda, waliona mazingira kuwa tayari kwa kutimiza tamaa ya miaka mingi ya kuiteka nchi hii.

Umuhimu wa kupinga uvamizi wa adui

Wakati huohuo ni lazima kuzingatia hoja hii ya msingi kwamba; kutimia kwa mwaka mmoja wa serikali ya Jolani pamoja na kuanza shughuli  za upinzani nchini Syria, kunatuma ujumbe wenye maana nzito sana  duniani na kwa wadau wa siasa na vita; kama alivyonukuliwa mchambuzi mmoja wa Kijordani na Al-Jazeera akisema:

“Ni uvamizi ambao unaulazimisha Muqawama, popote pale ulipo na kwa muda wote unapokuwepo katika ardhi ya wengine. Wasyria huko Beit Jinn walishinda kwa ajili ya ardhi na heshima yao, na hii ndiyo Syria tunayofahamu tangu mwanzoni mwa karne iliyopita, tangu nyakati za kupinga uvamizi wa kikoloni mfululizo. Upinzani wa kishujaa wa watu dhidi ya mashambulizi ya jeshi vamizi la Israel uliuweka upya dira ya Syria, na ukawa kama ukumbusho wa mwisho kwa Wasyria kwamba adui yao—aliyekalia ardhi yao na anayesimama mbele yao kama tishio kwa mustakbali, uwepo, ardhi na jamii yao—ni Israel, na Israel peke yake.”

Lengo la utawala wa Kizayuni ni nini!?

Utawala haramu wa Kizayuni katika hali ya sasa unatafuta kurudia uzoefu wa ukanda wa mpakani nchini Lebanon na pia nchini Syria; yaani, unataka eneo kutoka kusini mwa Damascus hadi mpaka wa Golan inayokaliwa, liwe eneo lisilo na majeshi na tupu, na pengine kuwasimamisha hapo machifu na mawakala wa ndani ili kusiwe na hatari wala tishio lolote kwa uwepo wa Israel. Hata hivyo, wavamizi wa Kizayuni kwa kuzingatia uzoefu wa miongo mingi ya kuishi katika eneo la Asia Magharibi wanapaswa kujua kwamba uvamizi huzaa upinzani, na si kwamba kwa kuwepo kwa serikali dhaifu na isiyo na busara ya Jolani wataweza kuwa na amani kutoka upande wa Syria.

Miundombinu iliyoharibiwa na madai yaliyokusanyika

Mwaka mmoja baada ya kuanguka kwa Bashar al-Assad, kilichobaki ni miundombinu iliyoharibiwa, ilhali nchi za Kiarabu pamoja na Uturuki bado hazijatekeleza kwa uzito ahadi zao za kuijenga upya Syria. Wataalamu wanakadiria gharama ya kuijenga upya Syria iliyoathiriwa na vita kuwa zaidi ya dola bilioni 200, na haipaswi pia kupuuziliwa mbali kwamba kwa vyovyote vile, hivi karibuni pia kipindi cha “fungate” cha Jolani na marafiki zake kitaisha, na atalazimika kuwajibikia katika madai yaliyokusanyika ya Wasyria.

Kwa sasa, watu wa Syria kutoka makabila na jamii mbalimbali, kwa kiwango kikubwa hawaridhiki na hali ya uchumi na huduma za umma, sambamba na kuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wao wa ndani. Kwa msingi huu, ni lazima kusemwa kwamba iwapo Jolani na timu yake hawataweza kushinda matatizo mengi ya kiuchumi, kijamii na kisiasa na kutoa mtazamo ulio wazi wa kuboresha hali, basi kuongezeka kwa migogoro ya ndani nchini Syria na kwa upande mwingine kuimarika kwa udhibiti wa Wazayuni, kutakuwa jambo linalowezekana kabisa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha