Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza A‘arafi, katika kongamano la mwaka la wawakilishi wa wanafunzi na wanazuoni wa Hawza nchini, lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Madrasa Ma‘asumiyya mjini Qom Iran, akielezea nafasi ya kihistoria na ya kiustaarabu ya Hawza alisema: Hawza ni taasisi ambayo kiasili ina tabia ya kiustaarabu inayojengwa juu ya fikra ya Kiislamu, na tabia hii imeendelea kwa zaidi ya miaka elfu moja.
Imam Khomeini alileta nadharia ya ustaarabu wa Kiislamu kwa mtazamo mpana na wa kishujaa
Mkurugenzi wa Hawza, akielezea mitazamo mitatu kuhusu ufahamu wa ustaarabu wa Kiislamu, alisisitiza: Imam Khomeini (ra) kwa kutoa tafsiri jumuishi, yenye mfumo, na inayokubali mabadiliko ya kielimu na kijamii, aliweka alama muhimu katika historia ya fikra za Kiislamu na kufungua hatua mpya katika maisha ya kiakili na kiustaarabu ya Uislamu.
Uislamu wa kiistaarabu; tafsiri jumuishi dhidi ya ufahamu potofu
Ayatullah A‘arafi, akirejelea tafsiri potofu kuhusu dhana ya Uislamu wa kiustaarabu, alisema: kuna kundi limeutafsiri Uislamu kwa namna kana kwamba vyanzo vya dini vinachukua nafasi ya fikra zote na juhudi za kielimu za binadamu, na inapaswa njia ya jitihada za kielimu ifungwe. Mtazamo huu, unaoonekana katika baadhi ya mikondo ya fikra pindukia na migumu, haukubaliki wala hauendani na uhalisia wa Uislamu.
Mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza aliongeza kusema: kinyume chake, tafsiri aliyowasilisha Imam Khomeini (ra) ni mtazamo jumuishi, unaojikita katika jamii na ustaarabu, unaozingatia nyanja zote za maisha ya binadamu, na wakati huo huo unakubali ukuaji na mageuzi ya kielimu pamoja na kujibu mahitaji mapya yanayojitokeza.
Kuzaliwa nadharia ya tatu; Usomaji mpya wa Uislamu mwanzoni mwa harakati
Mkuu wa Hawza, akirejelea miaka ya awali ya harakati ya Kiislamu, alikumbusha: ikiwa leo mtu atapitia fikra za Imam katika miaka ya 1341 hadi 1343 (Shamsia), hata hotuba, ujumbe na matamko, zile saba au nane chache za kipindi hicho, ataona wazi kwamba Imam, katikati ya Hawza, alikuwa akifanya uhakiki mpya na ujenzi mpya wa kina wa Uislamu katika nyanja za kielimu, kitamaduni, kijamii na kisiasa.
Alisema: wanazuoni wengi walikuwa wakielewa mtazamo huo, lakini hawakuwa na ujasiri au uwezo wa kuufuata. Kile kilichomtofautisha Imam ni kuunganisha kati ya ufahamu wa kina na wa kimfumo wa Uislamu na ujasiri wa kipekee katika kubainisha na kujenga mjadala wa kijamii. Sifa hizi mbili zilikusanyika kwa Imam Khomeini (ra), na hivyo nadharia ya tatu, yaani Uislamu wa kiustaarabu, ikaingia katika uwanja wa vitendo.
Athari za mtazamo wa kiustaarabu katika kazi za wanafikra wakuu
Ayatullah A‘arafi akirejelea athari za mtazamo wa kiustaarabu katika kazi za wanafikra wakuu wa Kishia, aliongeza: mizizi ya mtazamo huu inaonekana katika maandiko ya wengi miongoni mwa mabingwa wa fikra za Kiislamu. Katika kazi za wanazuoni wa fiqhi, teolojia, tafsiri, hekima na falsafa, mtazamo huu unaonekana wazi. Katika fikra za Allama Tabataba’i, iwe katika mijadala ya kifalsafa au katika tafsiri ya Al-Mizan, mtazamo wa kiustaarabu na jumuishi wa Uislamu umeakisiwa kwa uwazi.
Mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza aliongeza: hata hivyo, mtu aliyeyaunganisha mambo haya yote kwa kiwango cha juu, cha jumla na chenye mshikamano, na kuweka msingi wa harakati mpya, alikuwa Imam Khomeini (ra).
Imam Khomeini; Hatua yaenye mabadiliko katika mageuzi ya fikra za Kiislamu
Mkuu wa Hawza za elimu ya dini, akirejelea tathmini aliyoiwasilisha hivi karibuni kuhusu historia ya mageuzi ya Hawza katika mkutano wa wanazuoni wa Najaf, alisema: katika kipindi cha miaka 1200 iliyopita, zimetokea takribani nyakati kumi hadi ishirini za mageuzi ya kimsingi katika Hawza za elimu ya dini, ambapo wanazuoni wakubwa kama Allama Hilli, Khwaja Nasiruddin Tusi na wengine walikuwa wahusika wakuu, na kila mmoja wao aliunda hatua muhimu ya mabadiliko.
Aliendelea kusema: hata hivyo, Imam Khomeini (ra) alikuwa ni shakhsia ya daraja la kihistoria tofauti, aliyefanya mgeuko mkubwa katika historia. Alitumia turathi zote za nyuma, lakini akaanzisha mwendo mwingine; mageuzi ya karne nyingi yaliyoiingiza Uislamu katika hatua mpya.
Msingi wa mageuzi; Mzamo wa kiustaarabu wa Imam kuhusu Uislamu
Mkurugenzi wa Hawza za elimu ya kidini, akisisitiza kwamba kiini kikuu cha uadui dhidi ya Mapinduzi na fikra za Imam ni mtazamo huu wa kiustaarabu, alisema: roho na kiini cha mabadiliko yaliyoanzishwa na Imam Khomeini (ra) ni huo mtazamo mpana, wa kina na wa kiustaarabu kuhusu Uislamu. Mtazamo huu ni miongoni mwa misingi muhimj ya fikra za Kiislamu, ambao Imam aliuhuisha na kuuingiza katika uwanja wa kijamii na kisiasa.
Maoni yako