Alhamisi 11 Desemba 2025 - 07:00
Ushauri Muhimu wa Ayatollah Udhmaa Wahid Khorasani Kuwaelekea Vijana

Hawza/ Ayatollah Mkuu Wahid Khorasani amesisitiza kuwa: Ujana kwa mwanadamu ni kama msimu wa masika kwenye ulimwengu na katika mzunguko wa wakati. Katika msimu huu wa ujana, kila mbegu ya elimu na vitendo huzaa matunda.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Udhma Wahid Khorasani, katika kuwashauri vijana, amesema: Ujana kwa mwanadamu ni kama msimu wa masika katika ulimwengu na katika wakati. Katika kipindi cha ujana, kila mbegu ya elimu na amali huleta matunda; lakini uzee ni msimu wa baridi, na hakuna mbegu yoyote inayoweza kuzaa matunda katika kipindi cha baridi.

Enyi vijana! Tumieni fursa ya uhai kabla ya mauti, tumia vizuri ujana kabla ya uzee.

Baada ya msimu wa ujana kupita, hakuna kinachobaki isipokuwa majuto, kwamba: “Ningeweza kupata manufaa mengi kutoka katika maisha haya, lakini sikuyapata.”

Imenukuliwa kutoka katika maelezo  ya Ayatollah Udhmaa Wahid Khorasani.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha