Ijumaa 12 Desemba 2025 - 08:00
Lazima Kuzinduliwe Harakati ya Tafsiri ya Qur’ani

Hawza/ Mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi (Shura-ye Negahban), katika Mkutano wa Kitaifa wa "Mbebabendera ya Tafsiri", huku akisisitiza ulazima wa kuzinduliwa harakati ya tafsiri ya Qur’ani, alisema: “Leo Hawza ina darasa 250 za tafsiri kila siku, hiki ni kipindi kipya cha kuipa Qur’ani nafasi ya upekee.”

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami katika Mkutano wa Kitaifa wa "Mbebabendera ya Tafsiri" uliofanyika Alhamisi tarehe 11 December 2025 katika Jengo la Yawaran wa Hadhrat Mahdi (a.f.) jijini Qum Iran, pamoja na kubainisha nafasi tukufu ya Bibi Fatima al-Zahra (a.s.), nafasi ya tafsiri katika kuinua jamii ya kidini, na utumishi alio ufaya Hujjat l-Islam wal-Muslimin Qur'ati, alisisitiza ulazima wa kuanzishwa harakati madhubuti ya tafsiri ya Qur’ani ndani ya Hawza na nchini kwa ujumla.

Miaka hamsini ya kusuhubiana na Hujjat al-Islam wal-Muslimin Qar'ati

Imamu wa Ijumaa wa muda wa Tehran, huku akigusia historia ndefu ya kujuana kwake na Ustadh Qar'ati, alisema: “Urafiki wangu na ustaadh Qar'ati ni miaka hamsini kamili; kuanzia mwaka 1354 shamsia, hadi leo, huu si muda mfupi, tangia siku ya kwanza nilipomfahamu hadi leo, uchungu wa dini umekuwa ukidhihirika katika shakhsia yake—kuanzia Qur’ani, mpaka swala, mpaka zaka, na katika nyanja zote za kubainisha dini.”

Mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi (Majlis Khobregan Rahbari), akisisitiza ulazima wa kuipa tafsiri umuhimu mkubwa zaidi, alisema: “Qur'ani imedhulumiwa, lazima kuanzishwe harakati ya tafsiri — kazi endelevu, ya kina na ya pande zote, Hawza zinapaswa kuwa mstari wa mbele katika uwanja huu.”


Mbinu yake ya tafsiri

Ayatullah Khatami akabainisha mbinu yake ya tafsiri na kueleza: “Hatua ya kwanza ni kuiangalia aya inataka kusema nini. Qur’ani, kiistilahi na kibalagha, ni sayansi yenye ulazima. Lakini hapa kuna mitazamo miwili:

1. Mtazamo wa kwanza ni kuzama kupita kiasi kwenye lugha na balagha — mimi sipendelei hili;

2. Mtazamo wa pili ni kuangalia lugha na balagha kwa kiwango cha chini na cha kimatumizi, kwa kiasi ambacho uelewa wa aya unahitaji.”

Ulazima wa kurejea lugha asili

Ayatullah Khatami, akigusia kauli ya Ayatullah Al-Udhma Subhani, alisema: “Anasema: ‘Mufradat’ maana yake ni lugha; lakini ni lugha inayopaswa kuchukuliwa kutoka vyanzo asili na vya karibu na zama za Maimamu Ma‘sumin.”
Akawataja wakubwa kama Khalil bin Ahmad Farahidi katika kitabu cha "al-‘Ayn" na Ibn Faris katika kitabu cha "Maqayis al-Lugha" kuwa ni vyanzo vyenye thamani.

Akigusia kitabu "al-Tahqiq fi Kalimat al-Qur’an", alisema: “Marehemu Mustafawi alikiandika akitetea msimamo kuhusiana na kutokuwepo ‘neno lenye maana nyingi (mushtarak)’ katika Qur’ani. Ingawa kuna mjadala katika natija yake, lakini mkusanyiko wa maneno na mitazamo katika kitabu hicho ni wa thamani sana.”

Nafasi isiyoweza kufidiwa ya riwaya za Ahlul-Bayt (a.s.)

Ayatullah Khatami alisisitiza kuwa: “Hatuwezi kamwe kupuuzia riwaya za Ahlul-Bayt (a.s.). Qur’ani imeteremshwa katika nyumba yao.”
Aliongeza kuwa: “Kwa bahati nzuri zipo duru nyingi za tafsiri za ki-riwaya, kama tafsiri "ma’thur" kwenye juzuu 30 nchini Lebanon na pia Noor al-Thaqalayn, watu wa Sunna pia wana mkusanyiko wa juzuu 30 wa tafsiri ya riwaya. Kuzirejea ni jambo la lazima.”

Akaendelea kusisitiza: “Kila tunachosema kuhusiana na Qur’ani bado ni kidogo. Haki ya Qur’ani ni kubwa mno kiasi kwamba hata tukilalamika kuhusu kudhulumiwa kwake, haitoshi. Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: ‘Mola wangu! Kaumu yangu wameiita Qur’ani hii kitu kisicho na umuhimu.’ Lakini leo hatupaswi kama zamani kuishia kulalamika tu; mazingira yamebadilika.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha