Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kutokana na mnasaba wa maadhimisho ya kuzaliwa mwenye kheri na baraka Bibi Fatima Zahra, amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake, na kumbukumbu ya pili ya kufariki kwa “Mohsin wa Umma,” Ayatollah Sheikh Mohsen Ali Najafi (Mwenyezi Mungu amrehemu), kongamano la kumi na moja la kila mwaka la kimataifa la Taasisi ya Al-Kawthar lilifanyika huku mkubwa wa wanazuoni, wanafikra na wanafunzi wa elimu ya dini kutoka nchi mbalimbali wakishiriki, katika mji mtukufu wa Najaf Ashraf.
Ufafanuzi wa nafasi ya Fatimah
Kongamano hili la kielimu na kiroho lilifanyika kwa anuani ya “فاطِمَةُ بَضعَةٌ مِنّی” (Fatima ni sehemu itokanyo nami), na lilihudhuriwa na wawakilishi wa ofisi za Mara'ji Wakuu wa Taqlid, idadi ya watu mashuhuri wa kielimu na kidini wa Hawza Ilmiya ya Najaf Ashraf, pamoja na wageni kutoka nchi mbalimbali.
Mwenendo wa Bibi Fatima Zahra (a.s.)
Katika kongamano hili, Hujjatul-Islam Sayyid Rashid Al-Husseini, mhadhiri wa Hawza, alitoa hotuba iliyofafanua vipengele mbalimbali vya mwenendo mtakatifu na wenye nuru wa Bibi Fatima Zahra, amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake, na akaeleza kwa kina nafasi adhimu ya bibi huyo mtukufu katika mfumo wa fikra na itikadi ya Uislamu.
Kuwatunuku wahitimu wa Taasisi ya Al-Kawthar
Katika sehemu ya mwisho ya hafla, nyaraka na vyeti vya heshima vilikabidhiwa kwa wahitimu wa programu ya miaka minne ya tawi la Waidhin la Taasisi ya Al-Kawthar huko Najaf Ashraf. Aidha, viongozi wa taasisi hiyo, walitoa shukrani zao kwa kuhudhuria kwa wanazuoni, wageni na washiriki, mbali mbali na pia walitoa pongezi na shukrani kwa ushirikiano na msaada wao katika kufanikisha tukio hili la kielimu.
Kongamano hili lilihitimishwa kwa kusomwa Dua ya Faraj ya Hujja wa Mwenyezi Mungu, Imam wa Zama, Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake, na kuacha hali iliyojaa hali ya kiroho na mshikamano wa Kifatimah kwa mwa washiriki.
Maoni yako