Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Katika maelezo yao, wawakilishi wa koo za Amazigh walisema kuwa; dhumuni la ziara hiyo lilikuwa ni kuimarisha umoja na mahusiano miongoni mwa makundi mbalimbali ya kikabila, pamoja na kuimarisha mshikamano ndani ya Umma wa Kiislamu kwa ujumla. Waliongeza kuwa ziara hiyo ilikuwa ni tamanio la muda mrefu, ambalo hatimaye limetimia kwa mapenzi na matakwa ya Mwenyezi Mungu.
Kwa upande wake, Sheikh Ibraheem Zakzaky aliwakaribisha wageni hao na kuwashauri kushikamana na busara na diplomasia katika mahusiano yao na watu wengine. Pia aliwasisitizia kuwa; Waislamu ni ndugu wao kwa wao, na akawaonya wawe waangalifu dhidi ya njama za maadui wanaolenga kupandikiza mifarakano, fitna na migawanyiko miongoni mwao.









Maoni yako