Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa Bibi Zahraa (as), zilifanyika kwa siku tatu mfululizo, huku shughuli hizo zikizojumuisha michezo kwa watoto, maonesho ya biashara kwa wamiliki wa biashara, majadiliano kuhusu maisha ya Sayyida Zahra (as) na mchango wake katika kupinga unyanyasaji na dhuluma, ushairi kutoka kwa washairi, na maandamano miongoni mwa shughuli nyingine.
Katika siku ya kufunga sherehe hizo, kiongozi, Sheikh Ibraheem Zakzaky, alihudhuria tukio hilo na kuwaelezea hadhira kuhusu maisha ya Sayyida Zahra, nafasi yake ya heshima miongoni mwa wanawake wa ulimwengu, na jinsi alivyoishi baada ya kufariki baba yake, Mtume wa Allah (saww).








Maoni yako