Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Iran leo ilikuwa imejaa nuru na furaha kutokana na kukumbuka siku ya kuzaliwa Bibi Fatima Zahra (a.s.). Kwa mnasaba huo, katika Husayniyya ya Imam Khomeini (r.a.), mbele ya Kiongozi wa Mapinduzi na maelfu ya wanaowapenda Ahlul-Bayt (a.s.), mkusanyiko wenye hamasa ya kaswida, ushairi wa kidini na utenzi wa kumtukuza Bibi wa wanawake wote wa ulimwengu ulifanyika.
Ayatullah Ali Khamenei, katika hafla hiyo iliyoendelea kwa takribani saa tatu, kwa ajili ya kupongeza kuzaliwa kwa Bibi Fatima Zahra (a.s.), alisema: Watu wa Iran kwa kusimama kwao kidete kitaifa, wamezishindisha juhudi za kudumu za adui za kutaka kubadili “utambulisho wa kidini, kihistoria na kiutamaduni” wa taifa hili; na leo, pamoja na ulazima wa kupanga vyema mfumo wa ulinzi na mashambulizi katika kukabiliana na shughuli za ufikishaji wa kimtandao za adui zinazolenga “akili, nyoyo na itikadi”, Iran pendwa licha ya matatizo na uhaba unaoonekana kote nchini, inasonga mbele.
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi akiheshimu mjumuiko wa siku ya kuzaliwa Imam Khomeini (r.a.) na kuzaliwa Bibi Fatima Zahra (a.s.), alisema kwamba; fadhila na sifa za Bibi wa dunia mbili ziko juu kuliko uwezo wa mwanadamu kuzielewa. Akaongeza kusema: Pamoja na yote hayo, ni lazima kuwa wa kifatima — na kumfuata Bibi huyo wa kuigwa katika nyanja zote: Ucha Mungu, kudai haki, jihadi ya kubainisha ukweli, kuwa mchamungu katika ndoa, kulea watoto, na maeneo mengine yote ya maisha.
Akaeleza kuwa ushairi ni jambo lenye athari kubwa sana, akasisitiza kuwa: Ni lazima kupitia utafiti na uchunguzi wa kina kufanyiwa tathmini, kutambua changamoto, na kutafuta njia za kuimarisha na kukamilisha vipengele vyote vya jambo hili la ajabu.
Ayatullah Khamenei, akibainisha maendeleo makubwa ya ushairi kulinganisha na siku za nyuma, alisema ushairi ni miongoni mwa ngome za fasihi ya muqawama. Akaongeza: Kila fikra au harakati isiyokuwa na fasihi yake maalumu, huangamia taratibu. Ushairi kwa kuunda, kueneza na kuhamisha fasihi ya muqawama, wanaimarisha hitaji hili la msingi.
“Muqawama wa kitaifa” ni kusimama thabiti mbele ya aina zote za shinikizo
Kiongozi wa Mapinduzi alifafanua “muqawama wa kitaifa” kuwa ni uvumilivu na kusimama imara katika kukabiliana na kila aina ya mashinikizo ya wenye kutaka kutumia nguvu. Alisema:
Mara nyingine shinikizo ni la kijeshi— kama lilivyoonekana wakati wa Vita vya Kulazimishwa, na kama vijana walivyoliona katika miezi ya karibuni — na wakati mwingine ni la kiuchumi, kimtandao, kitamaduni au kisiasa.
Akaendelea kueleza kuwa; propaganda, makelele na fitna za vyombo vya habari vya Magharibi na viongozi wao wa kisiasa - kijeshi ni alama ya shinikizo la ufikishaji.
Lengo la mashinikizo mbalimbali ya mfumo wa ubeberu dhidi ya mataifa — hasa Iran — wakati mwingine ni upanuzi wa maeneo ya kiutawala, kama Marekani inavyofanya leo Amerika ya Kusini; wakati mwingine ni kutaka kutwaa rasilimali za nchi; na mara nyingine kubadili mtindo wa maisha; na muhimu kuliko yote, kubadili utambulisho.
Akigusia historia ya zaidi ya miaka mia moja ya juhudi za kimabavu zilizofanywa duniani ili kubadili utambulisho wa “kidini, kihistoria na kiutamaduni” wa Iran, alisema: Mapinduzi ya Kiislamu yamesababisha juhudi hizo zote zishindwe. Na katika miongo ya karibuni, taifa kwa kukataa kusalimu amri na kusimama imara mbele ya shinikizo linaloendelea la adui, limesambaratisha mipango yao.
Alisema kuwa; kuenea kwa dhana na fasihi ya muqawama kutoka Iran hadi mataifa mengine ya eneo na nchi zingine kadhaa ni ukweli ulio wazi. Akaongeza pia: Kazi nyingi ambazo adui amejaribu kuzifanya dhidi ya Iran, kama angezifanya dhidi ya nchi nyingine yoyote, taifa hilo lingekuwa limetoweka kabisa.
Ayatullah Khamenei akiashiria kuwa athari ya ushairi wa Zainabiyya katika kuibakiza kumbukumbu ya mashahidi na kuimarisha dhana ya muqawama ni kubwa sana, alisema: Leo sisi tuko zaidi ya mapambano ya kijeshi; tupo “katikati ya vita vya ufikishaji wa kimtandao” dhidi ya jeshi kubwa la adui, kwa sababu adui ameelewa kuwa nchi hii ya kimungu haiwezi kuyumbishwa wala kutwaliwa kwa shinikizo la kijeshi.
Akaongeza kuwa: Baadhi ya watu kila mara hutaja uwezekano wa kurudia vita vya kijeshi, na wengine kwa makusudi huchochea moto wa hofu kwa watu ili kuwaweka njia panda — lakini kwa idhini ya Mwenyezi Mungu hawatafaulu.
Kiongozi wa Mapinduzi alieleza kuwa “mkondo, hatari na lengo la adui” ni kufuta athari, malengo, na dhana za Mapinduzi na kuonesha zimekatwa kutoka kwa Imam Khomeini (r.a.).
Alisema Marekani iko katikati ya jeshi hili kubwa la adui, baadhi ya nchi za Ulaya ziko pembeni yake, na wasaliti na wapotevu wanaojaribu kujipatia maslahi Ulaya wapo pembezoni mwa jeshi hilo.
Akasema: Kama ilivyo katika uwanja wa kijeshi, katika vita vya ufikishaji wa kimtandao pia lazima kupanga safu yetu kulingana na mpangilio na malengo ya adui, na kujikita katika maeneo ambayo yeye ameyaweka kwenye shabaha—yaani “maarifa ya Kiislamu, Kishia na Kimapinduzi.”
Akaendelea kusema: Kusimama imara dhidi ya vita vya ufikishaji vya Magharibi ni vigumu, lakini inawezekana kabisa. Waimbaji washairi wanapaswa kuyafanya majukwaa kuwa ngome za kushikamana na thamani za Mapinduzi, na kwa kuthamini mapenzi ya vijana kwenye ushairi, wawakinge dhidi ya malengo ya adui mkaidi na muovu.
Kiongozi wa Mapinduzi aliendelea kutoa ushauri ufuatayo kwa washairi:
Mosi, Kubainisha mafundisho ya dini na mafundisho ya mapambano kwa kutegemea maisha ya Maimamu wote (a.s.);
Pili, Kushambulia maeneo ya udhaifu wa adui sambamba na kujibu shubha zake kwa uthabiti;
Tatu, Kuelezea dhana za Qur’ani katika nyanja za kibinafsi, kijamii, kisiasa na namna ya kukabiliana na adui.
Akaongeza kuwa; athari ya nauha (utenzi wa maombolezo) uliotungwa vizuri wakati mwingine huwa kubwa zaidi kuliko mihadhara na hotuba nyingi. Akawatahadharisha waimbaji: Wazingatie kwamba miziki na tamaduni za enzi za twaaghuti zisiingie katika majlis na mikusanyiko yao.
Katika hitimisho, Ayatullah Khamenei, huku akigusia kauli ya mmoja wa waimbaji kuhusu tatizo la vumbi huko Khuzestan, alisema: Hili ni mojawapo ya matatizo madogo tu; matatizo na uhaba katika nchi ni mengi, lakini taifa siku baada ya siku, kwa kusimama imara, ukweli, ikhlasi, nia njema na kudai haki, linauongezea Uislamu na Iran hadhi na nguvu. Kwa tawfiki ya Mwenyezi Mungu, nchi iko katika harakati, jitihada na maendeleo.
Katika sehemu ya mwanzo ya mkutano huo, waimbaji na washairi kumi na mmoja wa Ahlul-Bayt (a.s.) walisoma mashairi na kaswida.
Maoni yako