Ijumaa 12 Desemba 2025 - 06:00
Ayatullah Yazdi (r.a.) Alikuwa Mtu wa Zama Muhimu Katika Historia/ Mfano wa Hekima Katika Utendaji

Hawza/ Mkurugenzi wa Hawza katika hafla ya kufunga Mkutano wa Kitaifa wa “Vinara wa Harakati ya Kiislamu; Ayatullah Yazdi (r.a.)” alisisitiza: Mujaahid huyu wa kimapinduzi alikuwa kielelezo cha hekima katika utendaji, na shakhsia iliyokuwa na mchango muhimu katika zama muhimu za kihistoria na kijamii.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza A‘rafi katika hafla ya kufunga mkutano wa kitaifa uliokuwa na anuani isemayo “Vinara wa Harakati ya Kiislamu; Ayatullah Yazdi (r.a.)” iliyofanyika leo Alhamisi tarehe 11 December katika mji wa Qum Iran, huku akigusia nafasi tukufu ya mujaahid huyu wa kimapinduzi, alisema: “Daraja na hadhi ya Ayatullah Yazdi (r.a.) ni ya juu zaidi kuliko kile ambacho tumekifanya hadi sasa, na tunatarajia kuwa hafla hii ya kufunga isiwe mwisho, bali iwe mwanzo wa kuchukua hatua kubwa zaidi.”

Mkurugenzi wa Vyuo vya Kidini aliendelea kusema, huku akigusia mazingira ya miaka ya mwishoni mwa 1350 (miaka ya 1970) na kipindi chake cha masomo ya udini, na kuongeza: “Katika wakati huo tulikutana na sura mashuhuri kama Ayatullah Yazdi (r.a.). Yeye na wakubwa wengine wa Hawza kama Ayatullah Meshkini (r.a.) katika kipindi cha kukosekana Imam (Khomeini), walikuwa wakiongoza roho na fikra za Hawza.”

Kiunganishi kati ya Imam Khomeini (r.a.) na kizazi cha vijana

Mjumbe wa Baraza Kuu la hawza aliendelea kusema: “Katika wakati huo, licha ya kuwepo kwa maulamaa wakubwa na shakhsia mashuhuri, Ayatullah Yazdi (r.a.) alikuwa kiunganishi kati ya Imam Khomeini (r.a.) na kizazi cha vijana; watu waliokuwa wakipeleka fikra na mikakati ya Imam Hawza, na kutoka humo kuelekea vyuoni na katika jamii.”

Mwanachama wa Baraza la Wataalamu wa uongozi (Shura-ye Negahban) akibainisha umuhimu wa kuendelezwa harakati za fikra za Imam katika vizazi vya baadae alisema: “Nafasi ya uongozi na uelekezaji ya Ayatullah Yazdi (r.a.) na shakhsia mashuhuri nyengine za Hawza ndani ya taasisi ya Jami‘at Modarresin ilisababisha fikra angavu ya Imam kuendelea hata katika kipindi cha kukosekana kwake, na kupiga hatua katika vizazi vya vijana na watu wazima wa Hawza. Leo pia tunapaswa kuwashukuru wakubwa hawa wote.”

Msimamo wa Ayatullah Yazdi na vinara wa Hawza

Mkuu wa Hawza ya Qum, huku akisisitiza ukubwa wa shinikizo na mipaka iliyowekwa dhidi ya fikra ya Kiislamu, uhuru wa nchi na heshima yake, aliongeza kusema: “Watu walio tangulia katika kipindi kile, akiwemo Ayatullah Yazdi (r.a.), walistahimili ugumu wa udikteta wa ndani, ukoloni wa nje, na pia mwenendo wa uadui au kutojua ndani ya jamii. Msimamo huu ambao hauna mfano, ulikuwa ukiyeyusha milima, na ulikuwa ukiyeyusha ugumu wa miongo miwili ile.”

Mfano wa ghera katika dini na hekima kwenye utendaji

Ayatullah A‘rafi, akigusia hekima ya kiutendaji na wivu wa kidini wa marehemu Ayatullah Yazdi (r.a.), alisema: “Wivu wa kidini wa mtukufu huyu ulikuwa na vipengele viwili:”

Kwanza: Umakini na uangalifu dhidi ya uchafuzi na upotofu katika ngazi ya mtu binafsi, kijamii na katika uongozi wa nchi;

Pili: Kuwa na akili na busara zinazohitajika kwa ajili ya kuchukua hatua madhubuti.

Mtu mwenye hekima na umakini

Mkurugenzi wa Vyuo vya Kidini, akisistiza kuwa marehemu Ayatullah Yazdi (r.a.) alikuwa mtu mwenye hekima na umakini mkubwa, aliongeza kisema: “Wakati mwingine hudhaniwa kuwa hamasa yake ilitokana na hisia tu, lakini katika vikao mbalimbali ilionekana wazi kwamba hatua na misimamo yake yote vilifanyika kwa hesabu na mpangilio makini. Hamasa yake ya ndani na umakini wake wa nje vilikuwa vikiandamana na akili, mantiki na hatua za kiutendaji.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha