Ijumaa 12 Desemba 2025 - 00:00
Sheikh Al-Qattan Katika Kikao Chake na Jamil Hayek, Atilia Mkazo Kwenye Umoja wa Kitaifa na Kuliunga Mkono Suala la Palestina

Hawza/ Rais wa Jumuiya ya “Qawluna wa Al-Amal” nchini Lebanon, alipotembelea ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Amal mjini Beirut, alifanya kikao na Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati hiyo, Jamil Hayek.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ahmad Al-Qattan, Rais wa Jumuiya ya Qawluna wa Al-Amal na mwanazuoni wa Kisunni nchini Lebanon, alitembelea ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Amal mjini Beirut na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati hiyo, Jamil Hayek. Katika mkutano huo pia alikuwepo Sheikh Hassan Al-Masri, Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Amal.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, pande zote mbili katika kikao hicho walijadili mwenendo wa hali ya kisiasa ya ndani ya Lebanon pamoja na mambo ya kieneo, na wakasisitiza umuhimu wa kulinda na kuhifadhi umoja wa kitaifa na Kiislamu, kwa kuwa umoja huo ndio mdhamini wa maslahi ya Lebanon na wananchi wake.

Washiriki katika kikao hicho vilevile walilaani vikali mashambulizi ya kila siku dhidi ya Lebanon, na wakasisitiza ulazima wa kusimama  Walebanon wote katika safu moja ili kuzuia maadui kutumia fursa ya hali ya sintofahamu, na kusimamisha ukiukaji huu wa mara kwa mara wa mamlaka ya Lebanon katika anga na ardhi yake.

Katika sehemu nyingine ya mazungumzo yao, wahusika walisisitiza ulazima wa kuliunga mkono suala la Palestina, na kubainisha kwamba Palestina bado ni kadhia kuu ya ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu. Pia walitoa wito wa kusimama pamoja na wananchi wa Palestina katika kudai haki yao halali ya kuirejesha ardhi yao kutoka bahari hadi Mto wa Jordan.

Mwishoni mwa kikao hicho, Sheikh Ahmad Al-Qattan alimzawadia Jamil Hayek nakala ya kitabu chake kiitwacho:
“Mafhūmu al-Shart wa Ḥujjiyyatuh fī Ḍaw’i Ikhtilāf al-Usūliyyīn – Dirasah Muqāranah bayna al-Madhāhib al-Islāmiyyah”
(Mafhum ya sharti na uthibitisho wake kwa mujibu wa tofauti za wanazuoni wa fiqh uwe wa msingi – utafiti wa kulinganisha baina ya madhehebu ya Kiislamu).

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha