Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu wa Lebanon, katika taarifa yake baada ya kikao chake cha kila mwezi, ilionya kwamba ni lazima kujihadhari na mtego wa kile kinachoitwa “mazungumzo”; kwa sababu huenda yakajionesha kwa sura ya usalama au uchumi, lakini kwa malengo yake yakawa ya kisiasa na yenye kuelekea katika kuhalalisha uhusiano.
Jumuiya hiyo ilisisitiza: asili na hulka yetu ni ya Kiislamu, na kamwe hatutakubali kuhalalisha uhusiano, kwani kuhalalisha si sehemu ya tabia wala ya maumbile yetu.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa: Umma wa Kiislamu umekuwa lengo la mashambulizi mapana ya propaganda na hotuba, ambayo matokeo yake yamekuwa kushindwa na kudhoofika kisaikolojia; kwa namna ambavyo baadhi wameporomoka kimaadili na kiroho, wakaonesha udhaifu, wakasalimu amri, na wakadhani kwamba kujisalimisha mbele ya adui wa Kizayuni na kutii amri zake kunaweza kuwaokoa kutoka kwenye shimo la anguko walilonaswa nalo.
Katika sehemu nyingine ya taarifa hiyo imeelezwa: Hisia hii imetokana na habari za uongo, kupotoshwa kwa hali halisi, ripoti za kubuniwa za vyombo vya kijasusi vya Magharibi, kufanyika kwa makongamano, na matumizi ya mabilioni ya dola; sambamba na uenezaji wa uongo na kutia chumvi mambo, yote yakiwa na lengo la kueneza hofu na woga dhidi ya adui, na kwa upande mwingine kuwaonesha Waislamu kuwa dhaifu.
Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu kisha ikabainisha kwamba: Hapa ndipo nafasi yetu inapodhihirika; katika kusimama imara dhidi ya mvamizi na kufanya juhudi za kumtoa katika ardhi zote za Kiarabu na Kiislamu. Mvamizi huyu mporaji hajaridhika tu na kuikalia ardhi, bali pia ameikalia mioyo, akili na nafsi.
Taarifa hiyo ikaendelea kusema: Tunanuia kung’oa na kufuta kila athari na alama ya uvamizi huu, kwa namna ambayo hakuna utegemezi wala unyenyekevu utakaosalia, na wakati huohuo tunajivunia utambulisho na haiba yetu ya Kiislamu.
Mwisho, Jumuiya ilisisitiz kuwa: Suluhisho pekee ni kuondoka kwa mvamizi, kwani mvamizi huyu hataondoka kwa nguvu ya mazungumzo, bali ataondoka kwa nguvu ya silaha.
Maoni yako