Kwa mujibu wa Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, kundi la wanafunzi wa kiume na wa kike wanaosoma katika hawza za Kishia kwenye nchi za Iran, Iraq na Lebanon walifika nchini Nigeria na kumtembelea Sheikh Ibrahim Zakzaky, kiongozi wa Waislamu wa Kishia nchini humo, katika makazi yake mjini Abuja na kufanya nae mazungumzo. Pia yapaswa kufahamika kwamba, katika mkutano huu wa kirafiki, wanafunzi kutoka nchi za Niger, Mali na Burkina Faso walihudhuria pia.
Sheikh Zakzaky mwanzoni mwa kikao hiki alieleza kuwa lengo la mkutano huu ni kukumbushia umuhimu wa suala la ulinganizi wa kidini (tabligh) wa kuvuka mipaka, na akaongeza: chukueni kwa uzito suala la ulinganizi na wito wa haki, na katika maisha yenu yote jitahidini katika njia hii na muongeze maarifa yenu ya kielimu siku baada ya siku.
Aliendelea kusema: kutoa mawaidha pekee hakutoshi kutatua matatizo, kwani katika nchi nyingi za Afrika hatuna uhaba wa wahubiri (muballighina), lakini watu hawana mafungamano mazuri nao. Mawaidha ni mazuri na yana athari pale tu yanapokuwa na msingi wa kielimu na ushahidi, si kwamba mtu anataka kuwahubiria wengine bila kuwa na chochote mkononi.
Kiongozi wa Waislamu wa Kishia wa Nigeria, katika sehemu ya hotuba yake alizungumzia umuhimu wa kusoma na akaongeza: Mhubiri mwenye ufanisi hana haki ya kuhubiri na kuelekeza watu hadi awe amesoma vya kutosha. Kusoma na kutafuta elimu ni aina ya kujitolea, kwani mhubiri hutumia muda na nguvu zake katika kusoma na kujifunza, na katika njia ya elimu hujiteketeza kama kipepeo kinavyochoma mbawa zake kwenye moto.
Mhubiri huyu mujaahid katika sehemu nyingine ya hotuba yake, alisisitiza kusimama imara katika njia ya dini mbele ya madhalimu na waenezi wa bidaa, na akaongeza: jambo ambalo kwa sasa serikali na mawakala wa dhulma wanajaribu kulifanya lionekane la kawaida katika jamii ni suala la kuhalalisha mahusiano na madhalimu na wanyang’anyi wa haki za Waislamu. Tunapaswa kusema kuwa; sisi ni waendelezaji wa njia ya yule ambae katika hali mbaya zaidi na licha ya masaibu mengi na kuuawa kwa jamaa na wafuasi wake, hakukubali kudhalilika wala kuinama mbele ya dhulma na madhalimu.
Sheikh Ibrahim Zakzaky alihitimisha hotuba yake kwa kuwashukuru wanafunzi wa kiume na wa kike walio hudhuria kutoka hawza za ulimwengu wa Kishia, na pia kutoka nchi nyingine za Afrika katika mkutano huu, na alisisitiza umuhimu wa kueneza dini kwa lugha na lahaja mbalimbali, na akaeleza matumaini yake kuwa siku moja katika kila mtaa na jamii ndogo miongoni mwa mataifa ya Afrika kutakuwa na mhubiri na muongoza watu kuelekea kwenye ukweli.








Maoni yako