Jumanne 4 Novemba 2025 - 22:38
Juhudi za ukombozi za Roland Lumumba Zaheshimiwa nchini Kongo

Hawza/ Mkutano wa kielimu uliopewa jina “Madhara ya Ukoloni Barani Afrika” umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Kongo (UNICO) kwa ushirikiano na Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ukiwahusisha wasomi, maprofesa, wanadiplomasia na wanazuoni mashuhuri wa Kongo na Afrika.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Mkutano huo ulilenga kuchambua vipengele vya kihistoria, kitamaduni na kimaadili vya ukoloni na kuchunguza athari zake kwa jamii za Kiafrika. Miongoni mwa washiriki muhimu walikuwa Bwana Roland Lumumba (mwana wa hayati Patrice Emery Lumumba na rais wa Taasis ya Patrice Lumumba), Profesa Amouri Lumumba (mtafiti wa haki za binadamu na historia ya ukombozi wa Afrika), Profesa Crispin Kabasale Tshiamanga (mwalimu wa Chuo Kikuu cha Kinshasa na mwenyekiti wa chama cha U.D.S), pamoja na Bwana Hamidreza Anvari, mshauri wa kwanza wa ubalozi wa Iran katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Katika hotuba yake iliyokuwa na maudhui isemayo “Ukoloni na Uzembe wa Wasomi: Mgogoro wa Dhamiri ya Ulimwengu”, Dkt. Hussein Karbalaei, mwakilishi wa Taasisi ya Al-Mustafa huko Kongo na rais wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Kongo (UNICO), alisisitiza kwamba ukoloni wa kisasa hauonekani tena kwa nguvu za kijeshi, bali umevaa sura laini na tata zaidi kupitia uvamizi wa kifikra, kitamaduni na vyombo vya habari.
Akasema: “Ukoloni wa leo si nguvu ya nje, bali ni roho inayopumua ndani ya ukimya wetu.”
Aidha, alibainisha kuwa njia pekee ya ukombozi wa mataifa ni kufufua dhamiri ya kibinadamu na kuunganisha upya elimu na uhuru wa kweli.

Roland Lumumba, akiheshimu misingi ya ukombozi wa baba yake Patrice Lumumba, alisisitiza umuhimu wa kulinda uhuru wa kifikra na kitamaduni wa bara la Afrika.
Profesa Amouri Lumumba alitilia mkazo jukumu la vyuo vikuu katika kupambana na ukoloni wa kifikra, akisema kwamba uhuru ni jambo la ndani ya nafsi.
Profesa Crispin Kabasale, kwa upande wake, aliashiria kwamba taasisi za kifedha za kimataifa kama Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ni zana mpya za utawala wa kiuchumi na utegemezi wa Afrika.

Bwana Hamidreza Anvari, mshauri wa kwanza wa ubalozi wa Iran, alihutubia kwa muktadha wa maono ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, kuhusiana na uhusiano kati ya Magharibi na ulimwengu usio wa Magharibi.
Alifafanua kwamba mgongano na Magharibi si vita vya ustaarabu, bali ni mgongano wa mitazamo miwili kuhusu mwanadamu — mtazamo wa kwanza unaomwona mwanadamu kama chombo cha kutawala, na wa pili unaomwona kama kiumbe mwenye heshima na khalifa wa Mwenyezi Mungu duniani.
Aliongeza kuwa mataifa ya Afrika na ulimwengu wa Kiislamu yanapaswa kutumia utamaduni na maadili yao ya pamoja kurejesha uhuru wao wa kifikra, akisema: “Kama mataifa yataamini katika utambulisho wao, yataweza kubaki huru na yenye mamlaka kamili.”

Anvari pia alinukuu sehemu ya hotuba za Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu bara la Afrika, akibainisha kwamba uamsho wa mataifa ndio mwanzo wa mwisho wa enzi ya ukoloni.

Mwisho wa kikao hicho, Roland Lumumba alitunukiwa cheti cha heshima na uongozi wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Kongo (UNICO) kwa kutambua juhudi zake za kiutamaduni na uaminifu wake kwa urithi wa ukombozi wa Patrice Lumumba.

Juhudi za ukombozi za Roland Lumumba Zaheshimiwa nchini Kongo

Juhudi za ukombozi za Roland Lumumba Zaheshimiwa nchini Kongo

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha