Jumanne 21 Oktoba 2025 - 10:03
Je! Mlinzi wa eneo fulani, atawajibika kulipa mali za wakazi wa eneo hilo, iwapo wizi utatokea?

Hawza/ Mtukufu Ayatullah al-Udhma Khamenei amejibu swali la kifiqhi (istifataa) kuhusiana na hukumu ya kisheria, pale ambapo wizi utatokea katika makazi ya watu na ilihali kuna walinzi katika makazi hayo ambayo wizi huo umefanyika.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, katika mazingira shirikishi kama vile makazi, moja ya mambo yanayo leta wasiwasi mkubwa kwa wakazi na wasimamizi, ni juu ya uwajibikaji wa walinzi kuhusiana na mali za wakazi.
Swali hili limekuwa likulizwa mara kadhaa: Je! Kuwepo kwa mlinzi katika eneo fulani, kunamaanisha kwamba yeye ndie anawajibika moja kwa moja katika mali zote zilizopo katika eneo hilo (mdhamini kamili)? Mtukufu Ayatullah al-Udhma Khamenei ametoa jawabu kuhusiana na suala hili, kama ifuatavyo:

Swali:
Je! Katika makazi ya watu na mfano wake, iwapo mali za watu zitaibiwa. Je, mlinzi aliyekuwapo wakati wa wizi huo unafanyika atawajibika kwenye hasara hiyo (ni mwenye dhamana)?

Jawabu:
Iwapo mlinzi hakupuuza wajibu wake, basi hatokuwa ni mwenye dhamana (hotowajibika), isipokuwa kama katika mkataba wa ajira kulikuwa na sharti maalumu kuhusiana na jambo hili.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha