Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, hivi karibuni video moja imesambaa sana kwenye vyombo vya habari ikionesha wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Columbia wakipaza sauti dhidi ya vitendo visivyo vya kibinadamu vinavyo fanywa na utawala wa Kizayuni.
Kilicho cha kushangaza na cha kuvutia ni kwamba wanafunzi hawa, bila kujali vikwazo vilivyoanzishwa na Trump, kwa ujasiri mkubwa wanaunga mkono watu wanyonge wa Palestina.
Katika mwezi wa Machi, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Columbia waliendelea kuunga mkono watu wanyonge wa Palestina licha ya vitisho vya serikali ya Trump kwamba iwapo hawatakubali matakwa yake, mamilioni ya dola kutoka kwenye mfuko wao wa fedha wa shirikisho (federal fund) yatafutwa.
Katika ripoti za ndani ya nchi imeripotiwa kuwa zaidi ya waandamanaji 70 walikamatwa na polisi wa Columbia baada ya kupigwa na kushambuliwa, na mitandao ya kijamii ilisambaza upya vitendo hivyo vya kikatili vya polisi kwa kutumia hashtegi ya “ukandamizaji wa kikatili”.
Hii ni mara ya kwanza kwa Chuo Kikuu cha Columbia kufanya ukamataji tangu Aprili 2024, wakati ambapo waandamanaji wanaounga mkono Palestina walitoa kauli mbiu kwa karibu saa 24 katika chuo hicho.
Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, Chuo Kikuu cha New York kimekuwa kitovu cha maandamano ya wanaounga mkono Palestina dhidi ya vita visivyo na usawa na visivyo vya kibinadamu huko Ghaza, pamoja na upinzani dhidi ya msaada wa Marekani kwa utawala wa Kizayuni uanaomwaga damu za watu.
Maoni yako