Jumamosi 10 Mei 2025 - 19:53
Jana yenu isifanane na leo yenu / Matarajio ya kudhihiri Imam wa zama (a.j.f) kwa wanafunzi yazingatiwe ipasavyo

Hadhrat Ayatollah Makarem Shirazi, ameelezea majukumu mapya yanayoambatana na kuvaa rasmi vazi rasmi la kidini kwa wanafunzi wa Hawza na akasisitiza kuwa: Kuanzia leo mmepata haiba mpya, na haifai leo yenu iwe kama jana yenu; fahamuni kuwa kuvaa vazi hili kunampelekea Imam wa Zama (arwhuna fidaahu) anakuwa na matarajio kutoka kwenu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hadhrat Ayatollah Makarem Shirazi, katika hafla ya kuvaa rasmi vazi la kidini kwa kundi la wanafunzi wa Hawza ya Qom iliyofanyika katika ofisi yake kutokana na mnasaba wa kuzaliwa kwa Imam Ali bin Musa al-Ridha (a.s), alizungumzia karama na fadhila za mtukufu huyo na akasema: Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, kaburi la mtukufu huyo lipo katika nchi hii, na imekuwa ni hifadhi kwa wapendao na wenye shauku ya Ahlul-Bayt (a.s).

Yeye (Ayatollah) alisisitiza tena kuhusu majukumu mapya baada ya mwanafunzi kuvaa rasmi vazi la kidini, akasema: Kuanzia leo mmepata haiba mpya, na haifai leo yenu iwe kama jana yenu; fahamuni kuwa kuvaa vazi hili kunampelekea Imam wa zama (as) anakuwa na matarajio kutoka kwenu, na bila shaka atakuwa na uangalizi zaidi kwenu pia.

hadhrat Ayatollah alieleza kuwa, ikhlasi katika nia, nidhamu na juhudi za kudumu ni siri ya mafanikio kwa watu wengi mashuhuri, na akasema: Uchunguzi katika maisha na hali za wanazuoni na wakubwa wa dini ya kiislamu unaonesha kuwa misingi hii mitatu ndio sababu ya mafanikio yao.

Yeye pia alitaja tukio la kuadhimishwa miaka mia moja tangu kuanzishwa tena kwa Hawza, pamoja na kumbukumbu ya Ayatollah Hairi Qom, na akaongeza kwa kusema: Qom tangu enzi za Maimamu (as) imekuwa ni kitovu cha elimu na maarifa, na hayati Ayatollah Hairi aliweka msingi wa Hawza ya heshima, ambao unazidi kupanuka siku baada ya siku.

Mwisho wa hotuba yake, Ayatollah Makarem Shirazi aliwaombea wanafunzi hao dua, ili katika hatua yao mpya ya maisha waweze kutekeleza majukumu na wajibu wao kwa usahihi, na wawe miongoni mwa askari waaminifu na marafiki wa kudumu wa Imam wa zama (a.s).

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha