Jumatano 4 Februari 2026 - 10:00
Waandamanaji wa Kijerumani wametaka mateka waliopo katika magereza ya Israel waachiliwe huru

Hawza/ jiji la Berlin, mji mkuu wa Ujerumani, lilishuhudia maandamano ya mamia ya watu waliopinga ukiukwaji unaoendelea wa usitishaji mapigano na utawala wa Kizayuni. Waandamanaji hao pia walitaka kuachiwa huru kwa wafungwa wa Kipalestina kutoka katika magereza ya utawala huo.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, mamia ya waandamanaji walikusanyika katika Uwanja wa Oranienplatz mjini Berlin na kulaani kuendelea kwa mauzo ya silaha kutoka Ujerumani kwenda Israel. Pia waliwataka viongozi wa Israel kuwaachilia huru wafungwa wa Kipalestina na kumfikisha Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa Israel, mbele ya haki.

Waandamanaji, waliokuwa wakielekea katika kituo cha metro cha Südstern, walibeba bendera za Palestina pamoja na mabango yenye kaulimbiu kama vile: “Uhuru kwa Palestina”, “Israel inakiuka haki za binadamu”, “Simamisheni mauaji”, “Netanyahu mahakamani” na “Isusieni Israel”.

Miongoni mwa kaulimbiu muhimu zaidi za waandamanaji, ambazo zilisisitizwa kwa kiasi kikubwa, zilikuwa ni: “Uhuru kwa Palestina” na “Ghaza iko katika hali ngumu; maelfu ya watoto wameganda kwa baridi huko.”

Mwanzoni mwa wiki hii, Wapalestina 37 waliuawa ndani ya takribani masaa 24 katika mashambulizi ya anga ya Israel yaliyolenga maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Ghaza. Takribani raia wa Kipalestina milioni 2.4 wanaishi katika eneo hilo, wakiwemo wakimbizi milioni 1.5. Aina hii ya mauaji katika maeneo ya wakimbizi ni janga la kibinadamu.

Chanzo: Tovuti ya Habari ya Palestina

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha