Jumanne 3 Februari 2026 - 22:32
Usiku wa nusu ya Sha‘ban ni “Laylatul Qadr”

Hawza/ Mtukufu Ayatullah Jawadi Amoli wamesema: Imam al-Baqir (a.s.) amesema kuwa usiku wenye fadhila kubwa zaidi baada ya Laylatul Qadr ni usiku wa nusu ya Sha‘ban, usiku ambao Mwenyezi Mungu humiminia waja Wake fadhila Zake.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Mtukufu Ayatullah Jawadi Amoli katika hotuba yake ameizungumzia nusu ya Sha‘ban kama Laylatul Qadr ya Ahlul-Bayt (a.s.), na akabainisha kuwa: Kwa kuzaliwa Walii wa Mwenyezi Mungu, watu hunufaika na baraka bora zaidi; kwa sababu yeye ni kheri ya watu wa ardhini. Athari ya uwepo wa mtu bora zaidi katika ardhi huifanya ardhi yote na wakaaji wake wanufaike. Walii wa Zama (a.j.) na Hoja wa mwisho wa Mwenyezi Mungu, ambaye ni kheri ya watu wa ardhini katika zama zetu, alizaliwa alfajiri ya nusu ya Sha‘ban mwaka 255 Hijria. Usiku huu mtukufu, ambao ni usiku wa maadhimisho ya kuzaliwa kwake kwa furaha kubwa, huenda pia ukawa ni Laylatul Qadr, kama ambavyo pia baadhi ya amali za Laylatul Qadr zimependekezwa kufanywa katika usiku huu.

Nusu ya Sha‘ban ni usiku mtukufu ambao una fadhila nyingi zinazofanana kwa kiasi kikubwa na zile za nyusiku za Laylatul Qadr. Na kama ilivyonukuliwa kuhusu ubora wa nyusiku za Laylatul Qadr kwamba:

"فإنّها لیلة آلی الله علی نفسه الا یردّ سائلاً له فیها ما لم یسأل معصیة."

“Kwa hakika ni usiku ambao Mwenyezi Mungu Amejilazimisha Mwenyewe kwamba Hatamrudisha aliyeomba chochote ndani yake, muda wakuwa hajaomba jambo la maasi.”

Kauli nyingine yenye nuru kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) inaonesha kuwa nusu ya Sha‘ban pia, kwa kiwango chake, ni Laylatul Qadr na inabeba moja ya daraja za kupangiwa mambo. Katika kulinganisha sunnah hii na usiku mtukufu wa Laylatul Qadr, amesema:

"انّها اللیلة التی جعلها الله لنا أهل البیت بإزاء ما جعل لیلة القدر لنبینا صلی الله علیه و آله و سلم"

“Hakika huo ni usiku ambao Mwenyezi Mungu Ameufanya kuwa wetu sisi Ahlul-Bayt, sambamba na alivyoufanya usiku wa Laylatul Qadr kwa ajili ya Nabii wetu (s.a.w.w.).”

Kama vile Mwenyezi Mungu alimruzuku Mtume (s.a.w.w.) Laylatul Qadr, vivyo hivyo Ametutunuku sisi Ahlul-Bayt usiku wa nusu ya Sha‘ban.

Imam al-Baqir (a.s.), alipoulizwa kuhusu fadhila ya usiku wa nusu ya Sha‘ban, alijibu kuwa: usiku wenye fadhila kubwa zaidi baada ya Laylatul Qadr ni usiku wa nusu ya Sha‘ban, ambao Mwenyezi Mungu katika usiku huo huwapa waja Wake fadhila Zake na huwasamehe kwa ukarimu na neema Zake. Basi jitahidini kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika usiku huo, kwani Mwenyezi Mungu Ameapa kwamba Hatamnyima yeyote anayemuomba, mradi tu hajaomba jambo lisilofaa au dhambi:

هی أفضل لیلة بعد لیلة القدر؛ فیها یمنح الله تعالی العباد فضله و یغفر لهم بمنّه. فاجتهدوا فی القربة إلی الله (تعالی) فیها، فإنّها لیلة آلی الله تعالی علی نفسه ألا یرد سائلاً له فیها، ما لم یسئل معصیة و... فاجتهدوا فی الدعاء و الثناء علی الله (عزّ وجلّ).

“Ni usiku bora zaidi baada ya Laylatul Qadr; ndani yake Mwenyezi Mungu huwapa waja fadhila Zake na huwasamehe kwa neema Zake. Basi jitahidini katika kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu (Aliyetukuka) ndani yake, kwani huo ni usiku ambao Mwenyezi Mungu Amejilazimisha Mwenyewe kutomrudisha muombaji yeyote, maadamu hajaomba maasi… Basi jitahidini katika dua na kumsifu Mwenyezi Mungu (Azza wa Jalla).”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha