Jumatano 4 Februari 2026 - 07:00
Hizbullah katika eneo la Biqaa yatoa shukrani kwa Balozi wa Iran

Hawza/ Hizbullah katika eneo la Biqaa ilimuenzi Mojtaba Amani, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Lebanon, kwa mnasaba wa kumalizika kwa jukumu lake katika nchi hiyo, katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Utamaduni cha Imam Khomeini (r.a.) katika mji wa Baalbek.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hizbullah katika eneo la Biqaa ilimuenzi Mojtaba Amani, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Lebanon, kwa mnasaba wa kukamilika kwa misheni yake, katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Utamaduni cha Imam Khomeini (r.a.) mjini Baalbek.

Hafla hiyo ilifanyika sambamba na maadhimisho ya miaka arobaini na saba ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, na pamoja na Mojtaba Amani, Sayyid Hussein Mousawi, Naibu wa Kisiasa wa Katibu Mkuu wa Hizbullah na aliyekuwa mbunge wa zamani, pia alihudhuria.

Katika hafla hiyo, idadi ya watu mashuhuri wa kidini, kisiasa na kijamii walishiriki, wakiwemo: Hussein Al-Nemr (msimamizi wa Hizbullah katika eneo la Biqaa), Asaad Jaafar (msimamizi wa masuala ya kiutawala wa Harakati ya Amal katika Biqaa), Melhem Al-Hajjiri (mbunge), Hamad Hassan (waziri wa zamani), Mufti wa Hermel Sheikh Ali Taha, Anwar Jomaa, Sheikh Mashhour Sulh, Youssef Al-Yahfoufi (msimamizi wa eneo la Baalbek), Hussein Ali Raad (Mwenyekiti wa Muungano wa Manispaa za Baalbek), Ahmad Zuhair Al-Tufaili (Meya wa Baalbek) na naibu wake Abdulrahim Shalha, pamoja na wawakilishi wa vyama vya Lebanon, makundi ya Wapalestina, na wanaharakati wa kitamaduni na kijamii.

Hafla ilianza kwa kuimbwa wimbo wa taifa wa Lebanon, wimbo wa Hizbullah, na wimbo wa taifa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Baadaye, Ahmad Ria, msimamizi wa mahusiano ya umma wa Hizbullah katika eneo la Biqaa, huku akirejelea nyenzo za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, alisema: Mapinduzi ya Kiislamu tangu siku za mwanzo za ushindi wake, yalibeba bendera ya kuunga mkono kadhia ya Palestina; yalifunga ubalozi wa utawala wa Kizayuni na badala yake yakafungua ubalozi wa serikali ya Palestina; Imam Khomeini (r.a.) alianzisha Siku ya Kimataifa ya Quds na akasimama imara dhidi ya ubeberu wa Marekani. Leo pia, Imam Khamenei kwa ujasiri uleule, anatembea katika njia ya haki na kupambana na batili.

Akimzungumzia Mojtaba Amani, aliongeza: Kuagana nawe kunatuhuzunisha, lakini tuna yakini kuwa popote ulipo, utaendelea kumtumikia Mwenyezi Mungu na kufanya jihadi katika njia ya haki.

Hotuba ya Balozi wa Iran, Mojtaba Amani

Baada ya hapo, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mojtaba Amani, akitoa shukrani kwa waandaaji wa hafla hiyo, alisema: Nawashukuru kwa dhati ndugu na marafiki waliopanga hafla hii kwa ajili yangu sambamba na maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Najivunia kwamba Mwenyezi Mungu alinifanya niwe miongoni mwa waliojeruhiwa katika mapambano ya Bajar (Bejr) katika vita dhidi ya Israel — mbele ya utawala usio na ubinadamu, usiojua lolote isipokuwa uhalifu na uchochezi wa vita.

Aliongeza kuwa: Katika siku kama ya leo mwaka 1357 Hijria Shamsi, Imam Khomeini (r.a.) aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Tehran na akaanzisha miongo ya Alfajiri (Dahe-ye Fajr) na kuanguka kwa mpango wa Marekani katika eneo. Mapinduzi ya Kiislamu yaliwekewa msingi, na utawala wa Kizayuni wenyewe uliuita “tetemeko la ardhi dhidi ya Israel”. Tetemeko hili la kupinga dhulma bado linaendelea; japokuwa maadui kwa njama na vita mfululizo wanajaribu kuidhoofisha Jamhuri ya Kiislamu, wameshindwa, kwa sababu Iran imesimama pamoja na wanyonge wote wa dunia.

Amani alisisitiza: Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya bado zinafuata ndoto ya kutawala dunia, lakini Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, mataifa ya eneo na baadhi ya tawala huru, zimesimama dhidi ya dhulma hii, na kwa kutoa damu ya mashahidi, zinaendelea na njia ya haki.

Akiendelea kuzungumzia maendeleo ya hivi karibuni, alisema: Katika shambulizi la hivi karibuni dhidi ya Iran lililodumu siku 12, utawala wa Kizayuni haukupata mafanikio yoyote na hatimaye uliomba msaada wa Marekani. Jibu la Iran lilikuwa la kuitikisa ardhi. Sasa pia wanatishia kuishambulia tena, lakini wajue kuwa endapo uchokozi utarudiwa, hali hiyo hiyo itajirudia. Leo Jamhuri ya Kiislamu iko katika kiwango cha juu kabisa cha utayari, na uvamizi wowote utajibiwa mara moja na kwa uthabiti. Si Marekani wala Israel watakaopata chochote.

Katika mwendelezo wa hafla hiyo, Sayyid Hussein Mousawi, huku akisema kwamba mapambano kati ya haki na batili ni ya milele, alisema: Miongoni mwa sababu za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na harakati za muqawama ni: imani thabiti, umoja wa watu, uongozi wenye uelewa, kumtegemea Mwenyezi Mungu, utambulisho wa Kiislamu, uelewa wa kisiasa na kidini wa jamii, dhamira ya pamoja ya taifa, haki ya kijamii, na roho ya Husseini ya Imam Khomeini na Imam Khamenei. Thamani hizi ndizo zilizofanya damu ishinde silaha na dhulma.

Aliongeza kuwa: Wote wanapaswa kujua — hata Wale wanachi wa Lebanon walio na hofu juu ya Iran — kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran tangu mwanzo, imejitahidi kwa ajili ya uhuru wa Lebanon, si kwa ajili ya Mashia pekee, bali kwa watu wote wa Lebanon, na haijawahi kusita kutoa msaada. Sisi wafuasi wa Mapinduzi ya Kiislamu, tunamchukulia kila Mwislamu na Mkristo mwenye uzalendo kuwa ndugu yetu, na tunasimama naye bega kwa bega dhidi ya maadui wa taifa na Umma.

Alisisitiza pia: Haipaswi kusahaulika kwamba, Marekani na utawala wa Kizayuni ndizo sababu kuu za uharibifu wa nchi nyingi na hutafuta maslahi yao binafsi pekee; mfano ulio wazi ni mwenendo wa Donald Trump.

Mousawi alisema: Sisi ndani ya Hizbullah na Harakati ya Amal, pamoja na nguvu zote zilizo waaminifu, tutasimama kwa pamoja kuilinda Lebanon na Umma wa Kiislamu. Marekani inajaribu kutawala serikali na mataifa yote, lakini kama ilivyoshindwa huko nyuma, safari hii pia itashindwa.

Mwisho, aliwaita Walebanon wote walio huru kushirikiana katika kuzikomboa ardhi zilizokaliwa kwa mabavu, kuwaachilia wafungwa, na kujenga upya magofu, akisema: Tuko tayari kuwasilisha mkakati wa kitaifa wa ulinzi, ambapo muqawama utafanya kazi kwa mujibu wa maslahi ya taifa na nchi. Na kwa wale wanaochezea moto wa fitna za kikabila tunasema: sisi ni wale wale tuliotoa roho zetu kwa ajili ya kuwatetea Walebanon wote, Waislamu na Wakristo, na tutaendelea kuwa thabiti juu ya ahadi hiyo.

Katika hitimisho la hafla, Hussein Al-Nemr, msimamizi wa Hizbullah katika eneo la Biqaa, alimkabidhi Balozi Amani cheti maalumu cha heshima na shukrani.

Baada ya hapo, Balozi wa Iran na ujumbe wake walitembelea kaburi la shahidi Sayyid Abbas Mousawi, Katibu Mkuu wa zamani wa Hizbullah. Baada ya kusoma Al-Fatiha, Amani alisema: Sayyid Hassan Nasralluh, Sayyid Hashem Safi al-Din na mashahidi wengine wote walikuwa katika njia moja, na wamesimama imara juu ya njia hiyo ya Kiungu. Damu zao ni dhamana ya kuendelea kwa njia hii yenye nuru.

Sayyid Yasser Abbas Mousawi pia alisema: Katika siku kama hii, miaka 34 iliyopita — tarehe 12 Sha‘ban — baba yangu shahidi aliuawa kishahidi, na kama leo, ilikuwa siku ya Jumapili alasiri.

Tunamkaribisha balozi wetu mpendwa, na hatusemi “kwaheri”, kwa sababu amekuwa nasi daima; katika siku ngumu zaidi, katika huzuni ya kumpoteza Sayyid wa mashahidi wa Umma, Sayyid Hassan Nasrullah, Sayyid Hashem Safi al-Din na makamanda wengine mashahidi. Yeye pia ni miongoni mwa waliojeruhiwa katika mapambano ya Bejr, na tunajivunia ushirika huu.

Mwisho, kwa niaba ya familia ya Mousawi, zawadi za kumbukumbu zikiwemo tasbihi, pete ya fedha na nakala kadhaa za vitabu zilikabidhiwa kwa Balozi Amani.

Baada ya hapo, Balozi wa Iran alitembelea maqam ya Bibi Khawla (a.s.) mjini Baalbek, ambapo alipokelewa na uongozi wa haram na Sheikh Ali Farhat, na katika hitimisho, alikabidhiwa zawadi kutoka katika baraka za maqam hiyo tukufu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha