Shirika la Habari la Hawza - Mwenyekiti wa kamati ya amani ambae pia ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab, ameongoza kikao cha amani kilicho andaliwa chini ya Raisi wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ally Mwinyi, kikiwa na anuani ya kujadili mustakabali wa amani kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.
Katika kikao hicho mwenyekiti huyo wa amani Zanzibar amesema: Mkakati wa kamati hiyo ni kuhakikisha mazingira ya uchaguzi yanakuwa ya amani wakati wa uchaguzi, na baada ya uchaguzi, na wananchi waingie katika uchaguzi kwa uwazi, upendo na furaha.
Nae Rais Mwinyi ameihakikishia kamati hiyo kuwa, Serikali inafanya kila juhudi kuhakikisha mifumo yote ya uchaguzi inafanya kazi kwa uhuru ,Amani na uwazi wakati wa kampeni, upigaji kura na matokeo ya uchaguzi, kwa dhamira ya kudumisha amani iliopo kwa ajili ya maslahi ya nchi.
Dkt, Mwinyi ameishauri kamati hiyo kuwakutanisha wanasiasa na kufanya Mjadala wa pamoja ili Kuzungumzia umuhimu wa amani ya nchi pamoja na kudhibiti viashiria vya uvunjifu wa amani kabla na baada ya uchaguzi.
Maoni yako