Sayed Sajad Izdehi, mfuasi wa jopo la wanazuoni wa Tamaduni na Fikra ya kiislamu, katika mazungumzo na mwandishi wa shirika la habari la Hawza aliashiria kuhusu jukumu la kuongoza na kuendesha Hawza za Kiislamu, alisema: "Hawza ya Kiislamu ni ya kila zama, na inapaswa kutoa majibu kwa mahitaji yote, na inapaswa kupangwa na kupangiliwa ili iweze kusonga mbele kwa namna ambayo haitaacha nyuma mifumo ya utamaduni wa kisasa."
Mfuasi huyu wa jopo la wanazuoni wa Tamaduni na Fikra ya Kiislamu katika muendelezo wa mazungumzo yake akizungumzia kauli za Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya kiislamu, alisema: "Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ana usemi wa kwamba; "Hawza lazima iwe na mtazamo wa mbali, iwe na mifumo inayobadilika na iwe na maono ya baadaye ili isishindwe na muktadha wa kimagharibi."
Mwalimu huyu wa Hawza na chuo kikuu aliongeza kusema: "Masuala ya akili mnemba si tu ni teknolojia mpya, bali ni mlango mpya wa maarifa, na inapaswa kuzingatiwa kama mustakbali wa baadae.
Bila shaka, mfumo wa Kiislamu na Hawza ya Kiislamu, ambavyo vinadai kuwa na mchango katika utamaduni, vinapaswa kuzingatia jambo hili.
Ikiwa hatutatilia umuhimu akili mnemba, si tu mifano yake kama vile baadhi ya injini za utafutaji, roboti za majadiliano, nk, bali pia asili yake, na sisi wenyewe tusivitilie umuhimu, jamii itakuwa inaongozwa na mfumo ambao haulingani na mafundisho ya kiislamu.
Maoni yako