Shirika la Habari la Hawza - Sheikh Mubajje amesema hayo katika ujumbe wake wa Idul Fitri, ambapo pia ameeleza kusikitishwa na baadhi ya viongozi wa Kiislamu wanaotumia mitandao ya kijamii kutoa taarifa za upotoshaji kwa waumini.
Amesema mtandao wa TikTok ni mbaya zaidi hata kushinda mtandao wa Facebook ambao ulifungwa na serikali huko nyuma, na kwamba wakati umefika wa kuchukuliwa hatua ya ama kupiga marukufu au kuudhibiti mtandao huo.
Mapema mwezi uliopita wa Machi, Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kenya iliutaka mtandao wa kijamii wa China wa TikTok uondoe maudhui za kingono zinazowalenga na kuwaathiri watoto.
Kwa mujibu wa taarifa ya kiuchunguzi iliyotolewa na mamlaka hiyo, jukwaa la TikTok lilikuwa likipata faida kutokana na maudhui hizo za mambo machafu zenye kuhusisha watoto wenye umri wa miaka 15. Mtandao wa TikTok ndilo jukwaa la tatu kwa kuwa na wafuasi wengi duniani, likitanguliwa na Facebook na WhatsApp.
Maoni yako