Shirika la Habari la Hawza - Je! Unatafuta njia bora zaidi ya kumlea mtoto wako? Nguvu ya kuongea nae usiidharau! Kwa kuimarisha ustadi wako wa mazungumzo, unaweza kusaidia kurekebisha tabia mbaya za mtoto wako na kuepuka madhara ya muda mrefu yanayotokana na adhabu ya kumpiga.
Badala ya adhabu ya mwili, boresha ustadi wako wa kuzungumza nae.
Haijalishi tabia ya mtoto ni mbaya kiasi gani, kwa kuzungumza naye kwa upole, unaweza kumfundisha kwa kiasi kikubwa na akafahamu kwamba, tabia yake sio satahiki na inapaswa kurekebishwa.
Lakini kama tangia mwanzo utachagua kutumia nguvu na vipigo, si kwamba tu hautapata matokeo mazuri, bali itasababisha athari mbaya zaidi katika tabia ya mtoto kwenye maisha yake.
Maoni yako