Hujjatul Islam wal Muslimin Mohammad Hassan Zamani, mshauri wa mudiri wa Hawza nchini Iran katika masuala ya Ahlul-Sunna, alipokuwa akizungumza na Shirika la Habari la Hawza, alisema kuwa: Mapinduzi ya kiislamu ya Iran ni utimilifu wa ndoto ya Kishi’a, aliongezea kuwa, Imam Hussein (a.s.) hakufanya mapinduzi Karbala kwa ajili ya mambo madogo tu, bali alipaza sauti kuwa ikiwa utawala utaondoka katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi dini itapotea kabisa, akasema kuwa mapinduzi ya kiislamu ni mwendelezo wa ulingano huo wa Mbinguni.
Hujjatul Islam wal Muslimin Zamani, alieleza kuwa jamii kujitambua ni siri ya mafanikio, na akasisitiza kwamba: Iran kuyatangulia mataifa kama vile Marekani kwenye sekta ya ustawi wa jamii licha ya vikwazo walivyo navyo ni hatua kubwa na ya kipekee.
Mshauri wa Mudiri wa Hawza pia alimsifu kiongozi mkuu wa mapinduzi, na kumuelezea kama mfano wa kipekee wa uongozi wa kiislamu, pia alikumbushia kuwa: Mchanganyiko wa elimu ya kina ya fiqhi, werevu wa kisiasa, ujasiri mbele ya mabeberu, na maisha ya zuhudi umemfanya kuwa kiongozi wa kipekee katika ulimwengu wa kiislamu, sifa ambazo hata maadui wanazikubali.
Zaidi ya hayo, alizungumzia athari za kimataifa za mapinduzi ya kiislamu kwa kueleza kuwa, kuna wanafunzi elfu kumi kutoka mataifa 193 duniani wanaosoma katika vyuo vya dini nchini Iran hususan katika mji wa Qom, wanafunzi hao wakiwa ni mabalozi wa fikra nzuri ya Kishi’a.
Pia alisisitiza kuwa, jina la Iran na uongozi wake limekuwa ishara ya mapambano dhidi ya mabeberu katika maeneo ya mbali kama Afrika na Amerika ya Kusini, jambo ambalo linastahili pongezi.
Mwisho, alihimiza wananchi wa Iran kulinda urithi huu mkubwa na kuifanya Iran kuwa mfano wa kuigwa kimatendo katika ulimwengu wa kiislamu, alikumbushia pia maneno ya Kiongozi mkuu wa mapinduzi aliyesema kuwa; mapinduzi ya kiislamu yalikuwa ni mlipuko wa nuru, na nuru hiyo haitaweza kuzimwa hadi kudhihiri kwa Imam wa zama (a.s).
Maoni yako