Alhamisi 12 Februari 2026 - 17:30
Wafungwa wengi wa Kipalestina hawajasajiliwa katika magereza ya Israel

Hawza/ Suala la mauaji ya kimbari ya utawala wa Israel dhidi ya Palestina limeonesha pengo kubwa la kimaadili kati ya kauli za kibinadamu na utekelezaji wake. Kwa zaidi ya miaka miwili, idadi kubwa ya wafungwa wa Kipalestina katika magereza ya Israel wanaishi bila kusajiliwa katika chombo chochote rasmi na bila kupata huduma za matibabu.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, katika taasisi zinazoitwa za kibinadamu, kwa takribani miaka miwili majina ya wafungwa wengi wa Kipalestina walioko katika magereza ya utawala wa Kizayuni hayajasajiliwa rasmi. Wafungwa hawa waliosahaulika wanateswa na kunyimwa hata msaada wa msingi na huduma za matibabu.

Kwa maneno mengine, takwimu na habari zinaonyesha kuwa; katika baadhi ya matukio watu hawa wanahesabiwa kuwa wafungwa kwa baadhi ya taasisi za kimataifa, lakini hupotea na kufifia ndani ya takwimu za mauaji ya kimbari.

Vituo vya vizuizini vya Israel havishikilii wanaume pekee, bali pia wanawake, watoto na wagonjwa mahututi. Msongamano mkubwa, vurugu za kawaida, kunyimwa huduma za afya za kutosha na kusimamishwa ziara za familia ni mambo ambayo yameripotiwa kwa upana na kwa nyaraka.

Watetezi wa haki za binadamu na haki za Wapalestina wanaamini kuwa, ukimya huu si wa bahati mbaya. Wakati mateka wa Israel walitambuliwa haraka kama waathirika wa kimataifa, wafungwa wa Kipalestina — ambao idadi yao imefikia zaidi ya 9,000 — hata hawakupata utambuzi wa awali. Hakujakuwa na uchunguzi wa kimataifa wa dharura, wala juhudi za kidiplomasia za kudumu, wala hatua za dhati za kutekeleza viwango vya chini vya kibinadamu kwao.

Ripoti pia zinaonesha kuongezeka kwa vifo vya wafungwa walioko kizuizini, ambavyo katika miaka ya karibuni vinakadiriwa kufikia zaidi ya watu mia moja katika kila kipindi fulani cha muda kutokana na kupuuzwa kwa matibabu na matumizi mabaya ya huduma za afya.

Mashirika ya haki za binadamu yanaonya kuwa, nyaraka zilizopo zinaonesha sehemu ndogo tu ya ukiukwaji uliotokea.

Chanzo: SAFA NEWS

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha