Alhamisi 12 Februari 2026 - 18:30
Ghala la makombora la Iran linavunja utawala wa Marekani

Hawza/ Abdulkarim Khalaf alisisitiza kuwa ghala la makombora la Iran sasa limekuwa kizuizi halisi kwa kambi na meli za kivita za Marekani zilizopo katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Abdulkarim Khalaf, mtaalamu wa masuala ya usalama na kijeshi wa Iraq, alieleza kwamba ghala la makombora la Iran kwa sasa limegeuka kuwa kikwazo cha kweli kwa kambi na manowari za Marekani zilizowekwa katika eneo la Mashariki ya Kati.

Aliongeza kuwa; masafa ya makombora ya Iran, yanayozidi kilomita 3,000, yamefanya kina cha utawala wa Kizayuni na kambi zote za Marekani katika Ghuba ya Uajemi kuwa chini ya tishio la moja kwa moja.

Khalaf alisema: Kambi ya Al-Udeid nchini Qatar, ambayo ni kiini muhimu cha uongozi wa Kamandi ya Kati ya Marekani na ukuta wa kwanza wa ulinzi wa utawala wa Kizayuni, leo iko pamoja na kambi zinazofanana katika Falme za Kiarabu (UAE) na Kuwait ndani ya duara la kulengwa moja kwa moja kwa usahihi mkubwa.

Mchambuzi huyo wa usalama aliongeza kuwa; Washington imeweka meli za kijeshi kati ya 17 hadi 20 katika Ghuba, zikiwemo meli za kubeba ndege za kivita, lakini nguvu hii sasa inakabiliwa na changamoto nyeti mbele ya makombora ya balistiki na ya kasi kubwa (hypersonic) ya Iran.

Alibainisha kuwa; usahihi wa makombora ya Iran wenye kiwango cha makosa kisichozidi mita 10 umefanya mifumo ya ulinzi wa anga ya Marekani ishindwe kuyadhibiti au kuyazuia.

Khalaf aliendelea kusema: Kambi ya Harir kaskazini mwa Iraq, iliyotayarishwa kwa ajili ya kupokea vikosi vya anga, pamoja na kambi ya Al-Dhafra katika UAE, inayohifadhi ndege za kivita za F-35, zinachukuliwa kuwa malengo ya kimkakati katika hali yoyote ya mvutano wa kijeshi.

Mwisho, alieleza kuwa; nchi kama Saudi Arabia zinaweza kujiepusha na kuhusika moja kwa moja katika mgogoro wowote wa baadaye, kwa sababu zinatambua kuwa haziwezi kuhakikisha kikamilifu usalama wa malengo yao ya kijeshi katika makabiliano makubwa na Iran

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha