Alhamisi 12 Februari 2026 - 15:30
Iran inatekeleza nafasi ya unabii katika kukabiliana na Firauni wa zama hizi, yaani Uzayuni-Marekani

Hawza/ Mkondo wa Kiislamu wa Muqawama nchini Lebanon ulitoa pongezi kwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika maadhimisho ya miaka arobaini na saba ya ushindi wake, huku ukipongeza uongozi wake jasiri na taifa lake huru.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Mkondo wa Kiislamu wa Muqawama nchini Lebanon ulitoa taarifa rasmi kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 47 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, na ndani yake ukaipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, uongozi wake jasiri na watu wake huru kwa ushindi huo uliopatikana kwa damu na azma ya hiari yao, na ambao ulirejesha heshima, utu na nafasi ya Umma wa Kiislamu katika uwanja wa maisha baada ya kupotea kwa muda mrefu.

Katika taarifa hiyo imeelezwa kuwa: “Mnamo tarehe 11 Februari 1979, alfajiri ya uhuru ilichomoza kwa ushindi wa irada ya watu dhidi ya dhulma ya utawala wa kifalme. Siku hiyo ilibadilisha mkondo wa historia na kuthibitisha kuwa irada ya mataifa hushinda nguvu za matwaghuti; ilipuliza matumaini katika nafsi za waliodhulumiwa na kurejesha imani yao katika uwezo wao wa kufanya mabadiliko na kutoka katika utegemezi wa Mashariki na Magharibi kuelekea uhuru wa kweli; na ikaonesha Uislamu kama mfano wa utawala. Hivyo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikazaliwa.”

Taarifa hiyo inaendelea kusema: “Siku na miaka inapita, lakini Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na watu wake jasiri wameendelea kusimama imara mbele ya njama, hila na mzingiro unaolenga kuzima mwanga wa tajriba hii ya Kiislamu yenye kung’aa. Leo bado tuko katika duara la kushambuliwa, kwani shetani mkubwa — Uzayuni-Marekani — pamoja na vyombo vyake vya kimataifa, kikanda na vya ndani, wanajitahidi usiku na mchana kupitia hila zisizokoma kudhoofisha uthabiti na mafanikio ya mapinduzi haya yenye baraka na kuwatoa watu kutoka katika nuru kuelekea gizani.”

Mwisho wa taarifa hiyo umesema: “Mbele ya vitisho vinavyoikabili leo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, tunatangaza uungaji mkono wetu kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran; kwa kuwa nchi hii inatekeleza nafasi ya unabii katika kukabiliana na Firauni wa zama hizi, yaani Uzayuni-Marekani uliodhihirika kwa Donald Trump muasi. Tunatoa uwezo wetu wote kwa kumsaidia Mtukufu Ayatullah Khamenei (Mwenyezi Mungu amhifadhi), na tunamuomba Mwenyezi Mungu amlinde katika hifadha yake imara.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha