Ijumaa 21 Machi 2025 - 12:09
Mwaka wa "Uwekezaji katika Uzalishaji" / Mwaka wa 1403, Mwaka wa Kuonyesha Uwezo, Nguvu ya Mapenzi na Roho ya Juu ya Kiimani kwa Watu wa Iran

Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Khamenei, alitoa ujumbe wa mwaka mpya wa 1404 Hijria Shamsia, akitangaza kuwa mwaka huu utakuwa mwaka wa "Uwekezaji katika Uzalishaji."

Shirika la Habari la Hawza - Hadhrat Ayatollah Khamenei alikumbusha kuwa mwaka mpya unaanza wakati wa usiku wa Qadr na masiku ya kupata shahada Amir al-Mu’minin Imam Ali (a.s), akielezea matumaini yake kwamba baraka za usiku wa Qadr na huruma za Mola Mtakatifu zitakuwa pamoja na watu wa Iran na jamii yote inayo sherekea mwaka wao.

Alieleza kwamba mwaka wa 1403 ulikuwa ni mwaka wa matukio mengi yaliyojaa changamoto, akinukuu matukio kama vile shahada ya baadhi ya washauri wa Iran mjini Damascus, shahada ya Rais Raisii, Rais mpendwa wa taifa la Iran, na matukio mengine machungu yaliyo tokea Tehran na Lebanon, ambayo yalisababisha taifa la Iran na umma wa Kiislamu kupoteza baadhi ya watu muhimu.

Aliongeza kuwa vikwazo vya kiuchumi na changamoto za kimaisha, hasa nusu ya pili ya mwaka, ni miongoni mwa changamoto zilizoikumba Iran.
Alielezea kuwa; licha ya changamoto hizo, nguvu ya mapenzi, roho ya kiimani ya taifa la Iran, na mshikamano wa umoja vilijitokeza kwa wazi, hasa katika kukabiliana na msiba wa Raisii, wananchi walijitokeza kwa wingi katika mazishi, kuonyesha kuwa maafa haya hayakuweza kusababisha udhaifu katika taifa.

Alisema; kufanywa haraka kwa uchaguzi wa Raisi, ilikuwa ni ishara nyingine ya kuonesha uwezo wa kiimani kwa Wairani, ambapo nchi iliweza kutoka katika hali ya ukosefu wa uongozi na kuchagua Raisi mpya.

Pia alielezea juhudi kubwa za wananchi wa Iran kutoa msaada wa dharura kwa wananchi wa Lebanon na Palestina, huku akisema kwamba michango ya dhahabu kutoka kwa wanawake wa Iran ilikuwa ni moja ya matukio muhimu ya kihistoria ambayo yataendelea kuwa na kumbukumbu isiyosahaulika.

Ayatollah Khamenei alithibitisha kwamba nguvu na azma ya kweli ni mali muhimu kwa mustakabali wa Iran na itaendelea kuwa chanzo cha baraka za Mwenyezimungu kwa taifa hili.

Katika sehemu nyingine ya ujumbe wake, alikumbushia kuwa mwaka wa 1403 ulitangazwa kuwa "Mwaka wa Kukuza Uzalishaji kwa Kushirikiana na Watu," lakini alikiri kwamba licha ya juhudi za serikali, wananchi, na sekta binafsi, hali ya uchumi haikuruhusu kufikiwa kwa lengo hili kikamilifu. Alisema kuwa mwaka huu, suala kuu bado linahusu uchumi, hasa katika nyanja ya uwekezaji, kwani maendeleo ya uzalishaji na kutatua changamoto za kiuchumi yanahitajia uwekezaji katika uzalishaji.

Alisisitiza kuwa serikali ina jukumu la kuandaa mazingira ya uwekezaji kwa wananchi, na pale ambapo wananchi watashindwa kuwekeza serikali inaweza kuingilia kati na kufanya uwekezaji kama mbadala, lakini si kama mshindani wa wananchi.

Ayatollah Khamenei aliongezea kuwa ili uwekezaji katika uzalishaji utekelezwe, ni muhimu ipatikane dhamira ya dhati na motisha kutoka kwa serikali na wananchi. Alisema kuwa; kazi ya serikali ni kuondoa vizuizi vya uzalishaji na kuwawezesha watu kuwekeza kwa kutumia mitaji yao, ili mitaji hiyo isielekee katika mambo yasiyofaa kama vile fedha za kigeni na dhahabu.

Kiongozi wa Mapinduzi alimaliza ujumbe wake kwa kutangaza kuwa kauli mbiu ya mwaka 1404 ni "Uwekezaji kwa ajili ya Uzalishaji," akielezea matumaini yake kwamba; kupitia mipango ya serikali na ushirikiano wa wananchi, mabadiliko mazuri yatafanyika katika sekta ya uchumi na maisha ya watu.

Katika sehemu ya mwisho ya hotuba yake, Ayatollah Khamenei alilaani tena mashambulizi ya kikatili yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Gaza, akisema kuwa; hii ni jinai kubwa na janga ambalo linahitaji umoja na umma wa Kiislamu kwa pamoja kupinga vitendo hivyo.
Aliwataka watu wote walio huru duniani, kuungana dhidi ya jinai hii na kuzuia mauaji ya watoto na uharibifu wa mali.

Alisisitiza kuwa Marekani ni mshirika wa jinai hii, na alielezea kuwa mashambulizi dhidi ya watu wa Yemen ni jinai nyingine ambayo lazima isitishwe.
Alimalizia kwa kutuma salamu za kheri na mafanikio kwa umma wa Kiislamu, akiwatakia umoja wananchi wa Iran huku akitarajia Imam wa zama(a.j) na Roho ya Imam Khomeini (r.a) pamoja na mashahidi wa Iran ziwe radhi na watu wa Iran.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha