Alhamisi 3 Aprili 2025 - 18:36
Israeli yaua karibu watu 80 wa Gaza katika shambulio kwenye zahanati ya UN

Wimbi jipya la mashambulizi ya anga ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza yamesababisha takriban watu 77 kuuawa shahidi, ikiwa ni siku mbaya zaidi kwa Wapalestina tangu utawala katili wa Israel uanze tena mauaji yake ya kijinai na ya umati kwenye ukanda huo uliozingiwa kila upande.

 Shirika la Habari la Hawza - Kituo cha matibabu katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia kaskazini mwa Ghaza ni miongoni mwa maeneo yaliyoshambuliwa kikatili na utawala wa Kizayuni jana Jumatano.

Takriban watu 22, wakiwemo watoto na askari wa jeshi la polisi la Ghaza, wameuawa shahidi katika shambulio hilo lililpiga zahanati ya Umoja wa Mataifa.

Ofisi ya vyombo vya habari vya serikali huko Ghaza imelaani vikali shambulio la kinyama lililotokea wakati wa mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya raia na watu waliokimbia makazi yao huko Ghaza yakiendelea bila ya kusita.

Mashambulizi mengine kadhaa ya anga ya jana Jumatano yalipiga miji ya Khan Yunis na Rafah pamoja na kambi ya wakimbizi ya Nuseirat katikati mwa Ghaza.

Katika kuelezea hisia zake kupitia mtandao wa X leo ya Alkhamisi, Seneta wa Marekani Bernie Sanders ametangaza kwamba atalazimisha kupigwa kura ili kuizuia Marekani isiipe Israel shehena ya silaha ya dola bilioni 8.8.

"Israel imeshaua watu 50,000 huko Gaza na kujeruhi 112,000. Wiki mbili zilizopita, ilivunja makubaliano ya kusitisha mapigano na tangu wakati huo imeshaua watoto 322 na kujeruhi 600. Marekani lazima ikomeshe ushiriki wake," amesema.

Mashambulio hayo mabaya ya Israel yamekuja baada ya waziri wa vita wa Israel, Israel Katz kutishia kupanua mashambulizi ya Ghaza, akisema jeshi la utawala huo linnataka kuteka "maeneo makubwa" ya ardhi ya Palestina.

Israel ilianzisha mashambulizi ya kikatili ya umati dhidi ya wananchi wa Ghaza Oktoba 7, 2023, lakini ilishindwa kufikia malengo yake iliyotangazwa licha ya kuua Wapalestina 50,423, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto, na kujeruhi wengine zaidi ya 114,638.

Utawala wa Kizayuni ulilazimika kukubali masharti ya muda mrefu ya mazungumzo na Hamas Januari 19, 2025.

Lakini kuandia tarehe 18 Machi 2025, Israeli ilianza tena mashambulizi yake ya mara kwa mara huko Ghaza ikikanyaga kwa makusudi makubaliano ya kusimamisha vita.

Pars Today

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha