Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, katika mwanzo wa maadhimisho ya miaka arobaini na saba tangia ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuanza kwa sherehe za muongo wa Fajri, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, asubuhi ya leo (Jumamosi, tarehe 31 January 2026), alihudhuria katika kaburi tukufu la Imam Khomeini (rehma za Mwenyezi Mungu zimshukie) na kusoma Surat al-Fatiha, vilevile alitoa heshima kwa hadhi ya juu ya mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Imam Khamenei, baada ya kusoma Surat al-Fatiha na kuswali katika kaburi tukufu la Imam Khomeini (rehma za Mwenyezi Mungu zimshukie), alimwomba Mwenyezi Mungu ampe daraja za juu Imam huyo mkubwa na mpiganaji, pamoja na mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu.



Maoni yako