Jumanne 25 Machi 2025 - 11:47
Amirul-Muminin Ali (a.s) ni Qur'ani inayozungumza na ni mithili wa elimu ya Kimungu

Ayatollah Ulama alisema: "Imam Ali (a.s) mwenyewe alisema: 'Mimi ni Qur'ani inayozungumza," ambapo inamaanisha kwamba yeye ni Qur'ani inayosema kwa sauti, yeye ni mfano wa elimu ya Kimungu na ni ulimi wa Mwenyezi mungu, na maneno yake ni maneno ya Mwenyezi mungu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Ulama alieleza nafasi ya Imam Ali (a.s) katika mfumo wa uumbaji na uhusiano wake na Mtume Muhammad (saw) katika darasa la Akhlaq la mwezi wa Ramadhani lililofanyika ofisini kwa kiongozi mkuu wa mapinduzi, katika Husseiniya ya Imam Khomeini (r.a) huko Qom.

Alisema, akirejelea hadithi kutoka kwa Mtume Muhammad (saw) aliyosema: "Imam Ali (a.s) na mimi tumetokana na nuru moja," alisisitiza kwamba mtazamo wa Mtume (saw) na Imam Ali (a.s) ni sawa, na kwamba hawa wawili wapo katika kipimo kimoja cha mizani.

Ayatollah Ulama aliongeza kwa kusema: "Maasumin pekee ndio wanaoweza kusema juu ya ukweli wa uumbaji, daraja ya kimungu na cheo cha Irfani, kwa sababu wao wanafahamu uhalisia kamili juu ya uumbaji, na wale wasio na Maasumin kila watakavyo jitahidi kufahamu uhalisia huu, kamwe hawatapata ufanisi kamili wa ukweli huo."

Alipozungumzia nafasi ya Imam Ali (a.s) kama Qur'ani inayozungumza, alisema: "Imam Ali (a.s) mwenyewe alisema: 'Mimi ni Qur'ani inayozungumza', Yeye ni mfano wa elimu ya Kimungu na ulimi wa Mwenyezi mungu, na maneno yake ni maneno ya Mwenye mungu."

Ayatollah Ulama alielezea pia nafasi ya Salman al-Farsi kama mfano wa kufuata Qur'ani inayozungumza, kwa kusema: "Salman al-Farsi (r.a) kutokana na kumfuata Mtume Muhammad (saw) na Imam Ali (a.s), alifikia daraja ya Ahlul- Bayt (a.s), hii inaonyesha kwamba yeyote atakayekuja katika njia ya Qur'ani na Ahlul Bayt (a.s) atafikia daraja ya juu."

Mwalimu huyu wa Hawza pia alizungumzia tukio la Isra na Mi'raj la Mtume Muhammad (saw) na nafasi ya Imam Ali (a.s) katika tukio hili, kwa kusema: "Katika usiku wa Mi'raj, Mwenyezi Mungu alimuamuru Mtume Muhammad (saw) kuwauliza manabii wote kwa ajili ya nini walitumwa, wote walijibu kuwa walitumwa kuhubiri Tawhid, ujumbe wa Mtume wa Mwisho (saw), na uongozi wa Imam Ali (a.s), hii inadhihirisha ukubwa wa uongozi wa Imam Ali (a.s) katika mfumo wa kimungu."

Ayatollah Ulama kwa kuashiria hadithi kutoka kwa Abu Dharr al-Ghifari (r.a), alisisitiza: "Kumuangalia Imam Ali (a.s) ni ibada, Yeye ni kipimo cha matendo na mizani ya haki ya kimungu, na sisi tunapaswa kumchukulia Imam Ali (a.s) kama mfano kamili katika imani, maadili, na matendo yetu."

Alimaliza kwa kusema: "Sisi sote tunahitajia kabisa Ma'asumin, kwa sababu wao ni mfano kamili wa Wahyi na kioo kinacho akisi dhati ya Mwenyezimungu, na kwa kupitia wao pekee tunaweza kufahamu ukweli wa uumbaji."

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha