Jumanne 1 Aprili 2025 - 11:50
Umoja katika ulimwengu wa kiislamu ndiyo njia pekee ya kusimama dhidi ya uonevu unaofanywa na dola kubwa

Kwa mujibu wa shirika la habari la Hawza, kiongozi mkuu wa mapinduzi ya kiislamu, asubuhi ya leo hii, alipokutana na maafisa wa serikali, pamoja mabalozi wa nchi za kiislamu na wakiwepo na baadhi ya wananchi, alieleza kuwa heshima ya uislamu inazidi kuimarika, na kwamba kupambana na dhulma dhidi ya uonevu unaofanywa na madola makubwa kunategemea umoja na utambuzi wa umma wa kiislamu.  Pia alisisitiza kuwa Jamhuri ya kiislamu ya Iran inanyoosha mkono wa urafiki kwa serikali zote za kiislamu na akasema: "Njia madhubuti ya kukabiliana na jinai zisizo na kifani zinazofanywa na utawala wa Kizayuni na waungaji wake mkono huko Palestina na Lebanon ni mshikamano, umoja na uelewano kati ya serikali za kiislamu."  

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hadhrat Ayatollah Khamenei aliutakia umma wa kiislamu na taifa la Iran sikukuu njema ya Eid al-Fitr na akasema kuwa; Sikukuu hii ni moja ya nyenzo za kuwaunganisha waislamu na kuongeza hadhi ya uislamu na Mtume wake mtukufu, pia alibainisha kuwa sharti la kufanikisha hadhi hii ni umoja, azma, na utambuzi wa umma wa kiislamu.  

Akiashiria matukio yanayojiri duniani alisema kuwa, serikali za kiislamu zinapaswa kwa wepesi na umakini kubaini nafasi zao na kupanga mikakati inayofaa.  

Kiongozi wa mapinduzi, aliashiria fursa kubwa ambazo ulimwengu wa kiislamu unazo, ikiwemo idadi kubwa ya waislamu, utajiri wa maliasili, na nafasi yake muhimu kijiografia, na akasema: Ili kutumia fursa hizi ipasavyo, ni lazima kuwe na umoja wa kiislamu, alifafanua kuwa umoja huu haumaanishi kwamba serikali zote zinapaswa kuwa kitu kimoja au kuwa na mtazamo mmoja wa kisiasa, bali unahusu kutambua maslahi ya pamoja na kuyaainisha kwa namna ambayo haitasababisha migawanyiko na mifarakano.  

Alisisitiza kuwa ulimwengu wa kiislamu ni familia moja na serikali za kiislamu zinapaswa kufikiria na kutenda kwa kupitia mtazamo huu, Aliongezea kwa kusema: Jamhuri ya kiislamu ya Iran inajiona kama ndugu na mshirika wa serikali zote za kiislamu katika juhudi za pamoja.  

Hadhrat Ayatollah Khamenei pia alieleza kuwa ushirikiano wa serikali za kiislamu unaweza kuzuia dhulma, uonevu na unyang'anyi unaofanywa na dola zenye nguvu. Aliongeza kuwa leo hii, kwa bahati mbaya, uonevu dhidi ya serikali na mataifa dhaifu umekuwa ni jambo la kawaida kwa dola kubwa, Kwa hivyo, nchi za kiislamu zinapaswa kusimama kidete kutetea haki zao na kuizuia Marekani na mataifa mengine kufanya uonevu wa aina yoyote.  

Alihitimisha hotuba yake, kwa kugusia hali ya Palestina na Lebanon, alisema kuwa nchi hizi zinakabiliwa na mateso kutokana na jinai zinzofanywa na utawala wa Kizayuni na waungaji wake mkono, alisisitiza umuhimu wa ulimwengu wa kiislamu kusimama dhidi ya dhulma hizi na akasema kuwa: Kwa mshikamano na umoja wa serikali za kiislamu, mataifa mengine yatazingatia msimamo wa waislamu, alieleza matumaini yake kuwa viongozi wa nchi za kiislamu wataweza kutokana na juhudi na ari yao kuunda umma wa kiislamu kwa maana yake halisi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha