Shirika la Habari la Hawza - Kongamano la Qur'an Tukufu la 30 lililo simamiwa na Jamiatul Mustafa nchini Tanzania, limefanyika jana huku watu mbalimbali mashuhuri wakiweza kuhudhuria katika kongamano hilo.
Katika kongamano hilo ambalo liliwakilisha wasomaji mbalimbali mabingwa wa Qur'ani kutoka ndani na nje ya nchi ya Tanzania, liliweza pia kuhudhuriwa na viongozi tofauti kutoka taasisi mbali mbali za kidini na zile za kijamii pia.
Mabingwa wa kusoma Qur'ani, kutoka nchi mbali mbali wakifuatilia kwa karibu ratiba za hafla hiyo
Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna'asharia Tanzania (TIC), Sheikh Hemedi Jalala alikuwa ni miongoni mwa wahudhuriaji huku akiambatana na ujumbe wake maalumu kutoka katika Taasisi hiyo na hawza ya Imaam Sw'adiq (as). Vile vile, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Amani na Maridhiano (JMAT), Sheikh Alhad Mussa Salimu, nae pia ni miongoni mwa sura mashuhuri ambazo ziliweza kuhudhuria katika kongamano hilo, huku na yeye akiongozana na ujumbe wake maalumu. Pamoja na Balozi wa Irani nchini Tanzania nae pia alikuwa ni miongoni mwa wahudhuriaji katika Kongamano hilo.
Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna'asharia Tanzania (TIC), Sheikh Hemedi Jalala akiwa na baadhi ya washiriki katika hafla hiyo
Mgeni Rasmi katika kongamano hilo alikuwa ni Waziri wa mambo ya ndani Mheshimiwa Danieli Baran Sillo, ambae ukiachilia mbali furaha na bashasha ambazo zilimjaa kutokana na umahiri pamoja na uhodari wa wasomaji wa Qur'ani waliokuwa wakiuonesha, aliweza kuathiriwa sana na maneno adhimu ya Mwenyezimungu na hatimae mwisho wa kongamano hilo alikabidhiwa Qur'ani ikiwa ni zawadi kutoka kwa waandaaji wa kongamano hilo.
Maoni yako