Jumanne 20 Mei 2025 - 11:46
Mufti Mkuu wa Tanzania akutana na wanafunzi wa kitanzania katika ziara yake nchini Morocco

Hawza/ Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakr bin Zuber, amekutana na wanafunzi wa kitanzania nchini Morocco na kuweza kufanya nao mazungumzo ya pamoja.

Shirika la Habari la Hawza - Sheikh Abubakar Bin Zubeir Bin Ally ambae ndie Muft Mkuu wa Tanzania alifanya ziara yake nchini Morocco na kuweza kukutana na wanafunzi wa kitanzania ambao wanasoma katika Hawza ya Mfalme Muhamed wa sita nchini Morocco.

Ziara hiyo iliyofanywa na Mufti huyo wa Tanzania imekuwa ni tija ya uhusiano na mafungamano mazuri yaliyopo kati ya Mfalme wa nchi hiyo na Baraza la Waislamu nchini Tanzania (BAKWATA), Mfalme wa Morocco amekuwa ni mtu wa karibu mno na ambae ameweza kujitolea sana kwenye kuliwezesha Baraza kuu la Waislamu nchini Tanzania.

Katika ziara yake hiyo, Mufti mkuu wa Tanzania ameweza kuwahusia vijana wanaosoma nchini humo mambo matatu muhimu ambayo yeye ameyaita kama ndio muhimili mkubwa kwa kila mwanafunzi anaesoma elimu ya dini.

Jambo la kwanza, ni "mshikamano, ushirikiano na umoja", katika nukta hiyo Mufti Mkuu wa Tanzania amewataka vijana wanao soma hawza hiyo kuwa na umoja, mshikano na ushirikiano, kwani kwa kufanya hivyo wataweza kutengeneza mafungamano mazuri kati yako, nguzo kubwa ya kuwawezesha nyinyi kuondokana na upweke wa kukaa mbali na familia zenu ni kutengeneza uhusiano imara kati yenu, alisema Mufti huyo.

Pili, "kuweka bidii zote kwenye masomo", Mufti Mkuu wa Tanzania pia aliweza kuwahimiza vijana hao kuwa na bidii zaidi katika masomo, kwani hili ndilo lengo lao kuu ambalo limewapeleka katika nchi hiyo, na kuliacha hilo watakuwa ni wenye kukengeuka kuepukana na lengo lao.

Tatu, "kuwa na usikivu ugenini", miongoni mwa mambo muhimu ambayo Mufti wa Tanzania aliweza kuwahusia vijana wake ni "kuwa na usikivu wa hali ya juu wanapokuwa katika nchi za watu", mtu yeyote anapokuwa ugenini yampasa kuwa makini na kufuata kanuni na taratibu za nchi ile, kwani kila nchi ina kanuni na taratibu zake, hivyo yampasa kila mtu kufuata na kuheshimu taratibu za nchi husika ili asiweze kuingia katika matatizo.

Mwisho kabisa, vijana hao walionesha bashasha na furaha zao kwa kuweza kupata ugeni huo wa Mufti, na kusema kwamba; Imekuwa ni faraja mno kwao wao kwani wamejihisi kama vile wamekatana na familia zao. Hata hivyo waliweza kuwasihi vijana wenzao ambao wapo Tanzani kwa kusema kwamba; wawe mstari wa mbele pindi nafasi kama hizi za masomo zinapo tokea, na vile vile waliashiria kwamba nafasi hizi si kwa upande wa wanaume tu, bali wapo wanawake wengi pia ambao wanasoma masomo hayo ya dini katika Hawza hiyo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha