Jumatano 21 Mei 2025 - 08:46
Mitaa ya Lahaia yazingirwa na wapinzani dhidi ya vita

Hawza/ Waandamanaji waliovaa mavazi mekundu waliandamana siku ya Jumapili katika mji mkuu wa Uholanzi kwa lengo la kuitaka serikali yao kusitisha utekelezaji wa mikataba ya kibiashara na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, maandamano haya ya amani yaliyojumuisha zaidi ya watu 100,000 yalifanyika katika mitaa ya jiji la Lahaia, ambapo kwa mara hii vijana pamoja na watoto pia walikuwepo miongoni mwa washiriki wa maandamano haya.

Bi. Roos Lingbeek, mwalimu aliyehudhuria maandamano hayo, alisema: "Tunatumaini kwamba harakati hii kubwa yetu itakuwa pigo la kuamsha dhamira ya serikali."

Wakati huohuo, ripoti ziliripoti kuwa kwa masikitiko makubwa, Israel imeua karibia watu 103, wakiwemo watoto kadhaa, kupitia mashambulizi ya angani kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza.

Kuizingira wa Ghaza kunaofanywa na Israel pamoja na kufungwa kwa mipaka ya kivuko kunaendelea, huku wataalamu wa lishe na afya wakionya kwamba baa la njaa linatishia maisha ya watu milioni mbili katika eneo hilo, na iwapo hali hiyo haitashughulikiwa, inaweza kusababisha vifo vingi.

David Prinski, mmoja wa wanaharakati wanaoshiriki katika harakati hizi, alishiriki maandamano hayo huku akibeba picha ya tikiti maji lenye rangi za bendera ya Palestina. Katika mahojiano na shirika la habari la Associated Press, alisema: "Ninajiona kuwa na wajibu wa kushiriki katika maandamano haya na kusema dhidi ya dhulma."

Akaongeza kwa kusema:
"Tunaitaka serikali ya Uholanzi isitishe kila aina ya msaada — uwe wa kisiasa, kiuchumi au kijeshi — kwa Israel. Maadamu Israel inazuia watu wanyonge kupata misaada ya kibinadamu, Uholanzi, kwa kushirikiana nayo, inakuwa mshirika wa damu zilizomwagika."

Sera ya Uholanzi kuhusu Israel ni miongoni mwa masuala kadhaa yanayosababisha mpasuko kati ya serikali na muungano wa waandamanaji wa Kiholanzi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha