Shirika la Habari la Hawza - Imamu Ali, amani iwe juu yake, amesema:
«أَلاَ لاَ خَيْرَ فِي عِلْمٍ لَيْسَ فِيهِ تَفَهُّمٌ أَلاَ لاَ خَيْرَ فِي قِرَاءَةٍ لَيْسَ فِيهَا تَدَبُّرٌ أَلاَ لاَ خَيْرَ فِي عِبَادَةٍ لَيْسَ فِيهَا تَفَكُّرٌ.»
Tahadharini! Hapana kheri katika elimu ambayo, hapana ndani yake ufahamu. Tahadharini! Hapana kheri katika kisomo (kisomo cha Qur'ani) ambacho hapana ndani yake mazingatio! Tahadharini! 'Hapana kheri katika ibada ambayo hapana ndani yake kufikiria. (Al-Kafi ,J.1, Uk. 36)
Maelezo mafupi:
Kuujaza ubongo wa mtu kanuni za kisayansi, mantiki na falsafa, au elimu yoyote kutakuwa na athari ndogo sana hadi hapo kutakapokuwa na misingi ya fikra sahihi, mtazamo wa wazi ulimwenguni na kuitambua misingi ya maisha ya mwanadamu.
Ama usomaji wa Qur'an Tukufu utakuwa na athari ndogo iwapo hautaambatana na uchambuzi na kuzizingatia na kuzifikiria Aya zake, 'Ibada ambayo haina nuru katika ufikiriaji na busara ni sawa na mwili usio na roho, na kukosa athari za elimu ya hali ya juu.
Imenukuliwa kutoka katika kitabu kiitwacho "MAFUNZO 150 ya MAISHA BORA" - Ayatullah Makarim Shirazi
Maoni yako