Jumanne 20 Mei 2025 - 11:50
Siri ya kutokuwa bayana wakati wa kudhihiri Imamu wa Zama (as)

Hawza | Bila shaka yoyote, subira yenye tija ambayo ni miongoni mwa sababu kuu za harakati na uhai inajitokeza tu katika kivuli cha kufichika wakati wa kudhihiri Imam (as).

Shirika la Habari la Hawza - Mwenyezi Mungu Muweza na Mwenye Hekima, wakati wa kudhihiri umetufichwa. Na bila shaka, jambo hili lina hekima fulani ambazo baadhi yake tutazieleza hapa:

Kuendelezwa kwa Tumaini

Wakati ambapo wakati wa kudhihiri unakuwa umefichwa, mwangaza wa matumaini unabaki ndani ya nyoyo za wenye kungoja katika kila zama. Na ni kwa matumaini haya endelevu na yasiyokatika ndipo wanapoweza kuvumilia mashaka na misukosuko katika kipindi cha ghaiba. Kwa kweli, lau kama Waislamu wa karne zilizopita wangeambiwa kwamba kudhihiri hakutafanyika katika zama zao bali katika siku za mbele sana, wangekuwa na tumaini gani la kusimama imara dhidi ya fitina zilizokuwa zikifanyika zama zao? Na wangewezaje kuvuka salama njia za mashaka katika kipindi cha ghaiba?

Kuandaa Mazingira

Bila shaka yoyote, subira yenye tija ambayo ni miongoni mwa sababu muhimu za harakati na uhai, inajitokeza tu katika kivuli cha kufichika kwa wakati wa kudhihiri. Maana yake ni kwamba iwapo wakati wa kudhihiri ungefahamika, wale ambao wangetambua kuwa hawataishi hadi kudiriki kudhihiri huko, wasingekuwa na msukumo wa kuchangamka na kuandaa mazingira ya kudhihiri, bali wangeelekea kwenye uzembe na kudumaa.

Lakini hali ni tofauti, kwa kuwa wakati wa kudhihiri umefichwa, watu wa kila zama na nyakati wanajitahidi kuwa matumaini ya kwamba, huenda wakaushuhudia kudhihiri katika zama zao, hivyo basi, wanajitahidi kuandaa mazingira ya kudhihiri na kuigeuza jamii yao kuwa jamii yenye uadilifu na yenye uhai.

Zaidi ya hayo, ikiwa wakati wa kudhihiri ungewekwa bayana, na kisha kutokana na maslahi fulani kudhihiri kusingetokea katika muda huo ulio ainishwa, basi huenda baadhi ya watu wangeanza kuwa na shaka juu ya imani yao kwa Imamu (as). Kama ilivyoelezwa katika maneno ya Imamu Baaqir (as) alipoulizwa kuhusu iwapo kumeainishwa wakati maalumu wa kudhihiri, akasema:

«کَذَبَ اَلْوَقَّاتُونَ، کَذَبَ اَلْوَقَّاتُونَ، کَذَبَ اَلْوَقَّاتُونَ! إِنَّ مُوسَی عَلَیْهِ اَلسَّلاَمُ لَمَّا خَرَجَ وَافِداً إِلَی رَبِّهِ وَاعَدَهُمْ ثَلاَثِینَ یَوْماً، فَلَمَّا زَادَهُ اَللَّهُ عَلَی اَلثَّلاَثِینَ عَشْراً، قَالَ قَوْمُهُ: قَدْ أَخْلَفَنَا مُوسَی، فَصَنَعُوا مَا صَنَعُوا.»

Wanasema uongo wenye kuainisha wakati wa kudhihiri! WWanasema uongo wenye kuainisha wakati wa kudhihiri! Wanasema uongo wenye kuainisha wakati wa kudhihiri! Hakika ya Musa (as) alipoondoka kwenda kumuendea Mola wake kwa muda wa siku thelathini, na kisha Mwenyezi Mungu akaongeza juu ya zile siku thelathini siku kumi zaidi, kaumu yake wakasema: Hakika Musa ametukhalifui, na wakafanya walichokifanya. [yaani, walirudi nyuma katika dini na wakaabudu ndama.] (al-Kafi, juzuu ya 1, uk. 368)

Utafiti huu unaendelea...

Imenukuliwa kutoka katika kitabu kiitwacho "Negin-e Āfarinish" huku ikifanyiwa marekebisho kiasi

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha