Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya Tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, hafla ya kuwakumbuka mashahidi wa huduma ilifanyika nchini Nigeria. Katika hafla hiyo, shahidi Ayatollah Sayyid Ibrahim Raisi, ambaye tarehe 19 Mei mwaka jana alipata shahada kufuatia ajali ya ndege akiwa na baadhi ya wenzake, akiwemo mwakilishi wa Kiongozi wa Kidini Mkuu katika jimbo la Azarbaijan ya Mashariki na Waziri wa Mambo ya Nje, Hussein Amir-Abdollahian, alikuwa miongoni mwa shakhsia waliotukuzwa na kutambuliwa hadhi yao ya juu.
Katika hafla hiyo, wazungumzaji walitoa heshima kwa mashahidi hawa wakubwa na wakaomba msamaha na maghufira kwa ajili ya roho zao tukufu.
Mikusanyiko mingine ya aina hiyo pia iliandaliwa katika maeneo mbalimbali ya Nigeria.
Maoni yako