Jumatano 19 Machi 2025 - 06:30
Jumuiya za kielimu zina mchango mkubwa katika kutoa mawazo ya kimabadiliko katika Hawza za kidini

Tunaamini kuwa suala zima la kukuza, kustawi na mabadiliko katika Hawza lina misingi muhimu na nyeti, ambapo jambo hili linapaswa kuchunguzwa kwa kutumia akili ya pamoja na si kwa kujificha, ili liweze kutafitiwa kwa kina.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Arafi aliyazungumza hayo katika mkutano wa mwisho wa mwaka pamoja na wanajumuiya wa Taasisi za kidini kwa kusema: Taasisi za Hawza kutokana na mchango maalumu zilizokuwa nazo, zinaweza kuwa na athari kubwa na muhimu katika kuendeleza kasi ya mabadiliko katika Hawza na kuweka athari kwenye Hawza hizo, na sisi nguvu zote zinazotolewa na Taasisi hizi tutazitumia vyema.

Mjumbe huyu wa shura ya juu ya Hawza aliongeza kwa kusema: Tunaamini kuwa suala zima la kukuza, kustawi na mabadiliko katika Hawza lina misingi muhimu na nyeti, ambapo jambo hili linapaswa kuchunguzwa kwa kutumia akili ya pamoja na si kwa kujificha, ili liweze kutafitiwa kwa kina.

Mudiri huyo wa Hawza zote aliongezea kisema: Tangu zamani mchango wa Taasisi za Hawza katika miongozo ya kielimu na kiufundi haujawahi kujificha kwa mtu yeyote, lakini hapa tunalo ombi la kushirikiana, kufikiria kwa pamoja, pamoja na kuwa bega kwa bega na Taasisi hizi ili ziweze kutusaidia katika kuendesha ratiba na mipango kazi ambayo ipo katika ajenda za uongozi.

Ayatollah Araafi alisema: Jumuiya hizi ikiwa ni kama kama chanzo muhimu kwenye utafiti na ubunifu, zinaweza kutoa msaada mkubwa kwa viongozi na wapangaji wa ratiba mbalimbali za mageuzi na mabadiliko katika Hawza, ili tuweze kutumia uwezo huu mkubwa kwa manufaa ya mambo tofauti.

Mudiri huyo wa Hawza zote alimalizia kwa kusema: Taasisi zote hizi ni sehemu muhimu katika mfumo wa kielimu na utafiti wa Hawza, na zinashirikiana na uongozi wa Hawza katika kupangilia ratiba na miradi mbalimbali.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha