Jumanne 18 Machi 2025 - 05:34
Kusaidia Wanyonge wa Yemen ni Jukumu la Kisheria na Kibinadamu

Mwalimu wa Hawza ya Kiislamu ya Qom ameweka wazi kuwa: "leo hii ni jukumu la kisheria na kibinadamu kwa Waumini na Waislamu wote duniani kuisaidia Yemen ambayo inapigana Jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu katika kuilinda Ghaza.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Hawza, ujumbe kamili wa Ayatullah Seyfi Mazandarani ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Qasim wa mwiba wa wenye kuhujumu na muangamizaji wa madhalimu.

Nchi ya kihalifu ya Amerika, kwa mara nyengine tena ikiwa katika kuwakingia kifua Wayahudi wauwaji, imefanya uhalifu mwingine nchini Yemen.

Leo hii tunaona ishara za kiaga cha haki katika mapinduzi ya kipekee na ya wazi ya Yemen, mapinduzi ambayo yalianza miaka kadhaa iliyopita kukabiliana na mashambulizi ya kikatili yaliyo tokana na muungano mbaya wa Mawahabia, Marekani na Wayahudi, na watu mashujaa wa Yemen walikuwa mashahidi wa uhalifu mbaya zaidi, ubakaji, uharibifu wa miundombinu, na vilio vya kinamama pamoja na watoto.

Lakini Yemen shujaa haikurudi nyuma mbele ya uhalifu huu na dhulma hizi, bali inaendelea kushinda na kufikia mafanikio makubwa ambayo hayakutarijiwa, kwa kutumia silaha na zana za kisasa na zenye nguvu inasonga mbele katika vita.

Tunatumai kwamba kulingana na Hadithi za maimamu wa Ahlul Bayt (A.S), mapinduzi ya Yemen yataungana na mapinduzi ya Imam Mahdi (A.J) na bendera ya Yemen ambayo ni bendera ya kupigania dhulma, na kwa maelezo ya Hadithi mbali mbali, ni bendera inayofuata mwongozo wa kweli, na ni miongoni mwa bendera ambazo zitapeperushwa katika kipindi cha kudhihiri Hazrat Mahdi (A.J).

Leo hii ni jukumu la kisheria na kibinadamu kwa Waumini na Waislamu wote duniani kuisaidia Yemen inayopigana Jihadi kwa ajili ya Mwenyezimungu katika kuilinda Ghaza.

Jueni nyie na kutanabahi; hakika Nusura ya Mwenyezimungu ipo karibu.

Baraka za Mwenyezimungu na Mtume wake, na kila mumin na mja huru, na salamu za taifa shujaa la Iran kwa watu hawa jasiri.

Na salamu kwa watu wa Yemen wazalendo, wenye imani, na shujaa.
Mola awawafikishe kwenye kuinusuri dini yake na kuangamiza matwaghuti wenye kutakabari.

Mola atuwafikishe kwenye kuwanusuru wao.
Na amani iwe kwa waja wa Mwenyezimungu walio wema.

15 Ramadhani 1446

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha