Kwa mujibu wa ripot kutoka katika watarjumu wa Shirika la Habari la Hawza, Msako huu wa kuwakamata na kuwafukuza wanafunzi ni sehemu ya juhudi za serikali ya Donald Trump za kukandamiza wapinzani.
Marco Rubio, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, alieleza siku ya Alhamisi: “Tutafanya hivi kila siku, kila tunapompata mmoja wao tutaifuta visa yake, natumai siku moja watu hawa hawatakuwepo kabisa na tutakuwa tumewaondosha wote.
Kauli ya Rubio ilikuja baada ya kukamatwa kwa Romiz Ozturk, mwanafunzi wa udaktari kutoka Uturuki katika chuo kikuu cha Tufts, ambaye alikamatwa na maafisa wa uhamiaji karibu na nyumbani kwake Hapo awali, Ozturk alikuwa ameandika makala katika gazeti la chuo kikuu akiitaka taasisi hiyo kutambua vitendo vya utawala wa Israel huko Gaza kama mauaji ya kimbari.
Miongoni mwa waliokamatwa mwezi uliopita ni Mahmoud Khalil, raia wa Palestina mwenye hadhi ya ukaazi wa kudumu, na Badrakhan Suri, mtafiti wa baada ya udaktari kutoka India.
Maoni yako