Kwa mujibu wa shirika la habari la Hawza, mradi huu umechapishwa na Al-Hitra Foundation, chini ya Mwenyekiti wake Alhaj Mehboob Somji, ikiwa ni juhudi kubwa za kueneza elimu ya Qur’an na kukuza uelewa wa dini kwa jamii.
Hafla hii adhimu imehudhuriwa na viongozi mashuhuri akiwemo Alhaj Mohamedraza M Dewji, Rais wa Khoja, pamoja na viongozi wa Bakwata, Maulamaa na Masheikh kutoka madhehebu yote ya Kiislamu.
Hili ni tukio la kihistoria linalodhihirisha mshikamano wa Waislamu na umuhimu wa Qur’an katika maisha yetu. Kwa neema za Mwenyezi Mungu, Tafsiri hii itaongeza nuru ya elimu na kuimarisha imani zetu.
Maoni yako