Kwa mujibu wa ripoti kutoka katika Shirika la Habari la Hawza, Wosia wenye thamani kutoka kwa Ayatollah Kishmiri kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kiroho kila usiku ulijikita zaidi kwenye kutumia njia hii.
Ayatollah Kashmiri alisema:
Ni muhimu kutambua kuwa usingizi ni mfano wa mauti, na kila unapofika usiku mtu inatakiwa ajitayarishe kwa jambo hili.
Kwa kuifanya upya imani na ahadi yake kwa Mungu, mtu anatakiwa kutawadha, kuelekea Qibla, na kulala akimtaja Mwenyezi Mungu, aanze kwa kusoma Ayat Kursii, kisha afuate kwa kusoma Tasbihi za Bibi Zahra (a.s), na mwishowe atake msamaha kwa Mwenyezi Mungu.
Maoni yako